058-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kuingia Msikitini Baada ya Kula Kitunguu Thaumu au Maji au Karoti au Vitu Vyengine Vyovyote Vyenye Harufu Mbaya Kabla ya Kuondoka Harufu hiyo Isipokuwa kwa Dharura
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب نهي من أكل ثوماً أَوْ بصلاً
أَوْ كراثاً أَوْ غيره مِمَّا لَهُ رائحة كريهة عن
دخول المسجد قبل زوال رائحته إِلاَّ لضرورة
058-Mlango Wa Kukatazwa Kuingia Msikitini Baada ya Kula Kitunguu Thaumu au Maji au Karoti au Vitu Vyengine Vyovyote Vyenye Harufu Mbaya Kabla ya Kuondoka Harufu hiyo Isipokuwa kwa Dharura
Hadiyth – 1
عن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ أكَلَ مِنْ هذِهِ الشَّجَرَةِ - يعني : الثُّومَ - فَلاَ يَقْرَبَنَّ مَسْجِدَنَا )) . متفق عَلَيْهِ .
وفي روايةٍ لمسلم : (( مساجدنا )) .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kula mti huu - yaani thaumu (kitunguu saumu) - asiusongelee Msikiti wetu." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuwd].
Na katika riwaayah ya Muslim: "Misikiti yetu."
Hadiyth – 2
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ أَكَلَ مِنْ هذِهِ الشَّجَرَةِ فَلاَ يَقْرَبَنَّا ، وَلاَ يُصَلِّيَنَّ مَعَنَا )) . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kula mti huu asitusongelee wala asiswali na sisi." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن جابر رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ أكَلَ ثُوماً أَوْ بَصَلاً فَلْيَعْتَزلنا ، أو فَلْيَعْتَزِلْ مَسْجِدَنَا )) . متفق عَلَيْهِ .
وفي روايةٍ لمسلم : (( مَنْ أكَلَ البَصَلَ ، والثُّومَ ، والكُرَّاثَ ، فَلاَ يَقْرَبَنَّ مَسْجِدَنَا ، فَإنَّ المَلاَئِكَةَ تَتَأَذَّى مِمَّا يَتَأَذَّى مِنْهُ بَنُو آدَمَ )) .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kula thaumu au kitunguu maji ajitenge asiwe na sisi au auache Msikiti wetu." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy].
Na katika riwaayah ya Muslim: "Mwenye kula kitunguu maji na thaumu na karoti asiusogelee Msikiti wetu kwani Malaaikah wanaudhika kwa yanayo waudhi binadamu."
Hadiyth – 4
وعن عمر بن الخطاب رضي الله عنه : أنَّه خَطَبَ يومَ الجمْعَةِ فَقَالَ في خطبته : ثُمَّ إنَّكُمْ أيُّهَا النَّاسُ تَأكُلُونَ شَجَرتَيْنِ مَا أرَاهُمَا إِلاَّ خَبِيثَتَيْن : البَصَلَ ، وَالثُّومَ . لَقَدْ رَأَيْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، إِذَا وَجدَ ريحَهُمَا مِنَ الرَّجُلِ في المَسْجِدِ أَمَرَ بِهِ ، فَأُخْرِجَ إِلَى البَقِيعِ ، فَمَنْ أكَلَهُمَا ، فَلْيُمِتْهُمَا طَبْخاً . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa 'Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa alihutubu Siku ya Ijumaa akasema katika hotuba yake: "Kisha, hakika enyi watu! Nyinyi mnakula miti miwili ambayo siioni isipokuwa ni mibaya: Kitunguu maji na thaumu. Hakika nimemuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) pindi anaposikia harufu ya hivyo vitu viwili kutoka kwa mtu yeyote Msikitini, akiamuru atolewe apelekwe mpaka al-Baqi' (sehemu ya mbali). Hivyo, yeyote anayetaka kula vitu hivyo mwanzo azipike (ili aiondoe harufu yake)." [Muslim]