059-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Ihtibaa Siku ya Ijumaa Imamu Akiwa Ahutubu Kwani Linamletea Mtu Usingizi Hivyo Kukosa Kusikia Hotuba na Kuwa na Hofu ya Kutokwa na wudhuu

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب كراهة الاحتباء يوم الجمعة والإمام يخطب

لأنَّه يجلب النوم فيفوت استماع الخطبة ويخاف انتقاض الوضوء

059-Mlango Wa Ukaraha wa Ihtibaa Siku ya Ijumaa Imamu Akiwa Ahutubu Kwani Linamletea Mtu Usingizi Hivyo Kukosa Kusikia Hotuba na Kuwa na Hofu ya Kutokwa na wudhuu

 

Alhidaaya.com

 

عن مُعاذِ بن أنس الجُهَنِيِّ رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم نَهَى عَنِ الحِبْوَةِ يَومَ الجُمعَةِ وَالإمَامُ يَخْطُبُ . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقالا : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Mu'aadh bin Anas Al-Juhaniy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikataza Hibwah (ni mtu kukunja miguu yake na kuyaleta kwenye tumbo lake na kuyafunga na kitambara pamoja na mgongo wake na kukikaza) Siku ya Ijumaa Imamu anapohutubu." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Share