061-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kuapa kwa Viumbe Kama Nabiy, Ka'abah, Malaaikah, Mbingu, Baba, Uhai, Roho, Kichwa, Neema ya Sultani, Mchanga wa Fuani (Kaburi) na Amana, Nayo Imekatazwa kwa Ukali Zaidi
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن الحلف بمخلوق
كالنبي والكعبة والملائكة والسماء والآباء والحياة والروح
والرأس وحياة السلطان ونعمة السلطان وتربة فلان والأمانة ، وهي
من أشدها نهياً
061-Mlango Wa Kukatazwa Kuapa kwa Viumbe Kama Nabiy, Ka'abah, Malaaikah, Mbingu, Baba, Uhai, Roho, Kichwa, Neema ya Sultani, Mchanga wa Fuani (Kaburi) na Amana, Nayo Imekatazwa kwa Ukali Zaidi
Hadiyth – 1
عن ابن عمر رضي الله عنهما ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّ الله تَعَالَى يَنْهَاكُمْ أنْ تَحْلِفُوا بِآبائِكُمْ ، فَمَنْ كَانَ حَالِفاً ، فَلْيَحْلِفْ بِاللهِ ، أَوْ لِيَصْمُتْ )) . متفق عَلَيْهِ .
وفي رواية في الصحيح : (( فَمَنْ كَانَ حَالِفاً فَلاَ يَحْلِفْ إِلاَّ بِاللهِ ، أَوْ لِيَسْكُتْ )) .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah Anawakatazeni kuapia kwa baba zenu, mwenye kuapa basi amuapie Allaah au anyamaze." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]
Hadiyth – 2
وعن عبد الرحمان بن سَمُرَةَ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تَحْلِفُوا بِالطَّوَاغِي ، وَلاَ بِآبَائِكُمْ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abdir-Rahmaan bin Samurah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Usiape kwa Twawaaghiy wala kwa baba zenu." [Muslim]. Twawaaghiyt ni wingi wa Twaaghiyah nayo ina maana ya masanamu. Na miongoni mwayo ni Hadiyth: "Hili ni Twaaghiyah la Daws", yaani ni sanamu lao wanalo liabudu. Na imepokewa katika riwaayah isipokuwa ya Muslim: "Bit Twawaaghiyt", nayo ni mwingi wa Twaaghuwt yenye maana ya shetani na sanamu.
Hadiyth – 3
وعن بُريدَةَ رضي الله عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ حَلَفَ بِالأمَانَةِ فَلَيْسَ مِنَّا )) حديث صحيح ، رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .
Imepokewa kutoka kwa Buraydah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuapa kama amana si katika sisi." [Hadiyth Swahiyh iliyopokewa na Abu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]
Hadiyth – 4
وعن بُريدَةَ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ حَلَفَ فَقَالَ : إنِّي بَرِيءٌ مِنَ الإسْلاَمِ ، فَإنْ كَانَ كَاذِباً ، فَهُوَ كمَا قَالَ ، وإنْ كَانَ صَادِقاً ، فَلَنْ يَرْجِعَ إِلَى الإسْلاَمِ سَالِماً )) . رواه أَبُو داود .
Imepokewa kutoka kwa Buraydah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuapa, akasema: 'Mimi niko mbali na Uislamu, ikiwa ni muongo, basi atakuwa kama alivyosema na akiwa ni mkweli hatarudi katika Uislamu akiwa salama." [Abu Daawuwd]
Hadiyth – 5
وعن ابن عمر رضي الله عنهما: أنَّهُ سَمِعَ رَجُلاً يقُولُ: لاَ وَالكَعْبَةِ، فَقَالَ ابنُ عُمَرَ : لاَ تَحْلِفْ بَغَيْرِ اللهِ ، فَإنِّي سَمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقولُ : (( مَنْ حَلَفَ بِغَيرِ اللهِ ، فقد كَفَرَ أَوْ أشْرَكَ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa alisikia mtu akisema: "Naapa kwa Ka'abah." Ibn 'Umar akamwambia: "Usiape kwa asiyekuwa Allaah, kwani nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: 'Mwenye kuapa kwa asiyekuwa Allaah, hakika amekufuru au amefanya shirki'." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]