062-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uzito wa Kula Yamini Ya Uongo Kwa Makusudi
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تغليظ اليمين الكاذبة عمداً
062-Mlango Wa Uzito wa Kula Yamini Ya Uongo Kwa Makusudi
Hadiyth – 1
عن ابن مسعودٍ رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ حَلَفَ عَلَى مَالِ امْرِئٍ مُسْلِمٍ بِغَيرِ حَقِّهِ ، لَقِيَ اللهَ وَهُوَ عَلَيْهِ غَضْبَانُ )) قَالَ : ثُمَّ قَرَأَ عَلَيْنَا رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، مِصْدَاقَهُ مِنْ كِتَابِ الله عزوجل : [ إنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَناً قَلِيلاً أُولَـٰئِكَ لَا خَلَاقَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّـهُ وَلَا يَنظُرُ إِلَيْهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٧﴾] [ آل عمران : 77] . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuapa kiapo cha uwongo ili apate kuchukua mali ya mtu Muislamu pasi na haki, atakutana na Allaah akiwa Ameghadhibika naye." Akasema (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Kisha, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akatusomea aya katika Kitabu cha Allaah Ta'aalaa kuunga mkono kauli hiyo: '
إنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَناً قَلِيلاً أُولَـٰئِكَ لَا خَلَاقَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّـهُ وَلَا يَنظُرُ إِلَيْهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٧﴾
Hakika wale wanaobadilisha Ahadi ya Allaah na viapo vyao kwa thamani ndogo, hao hawana sehemu yoyote katika Aakhirah na wala Allaah Hatowasemesha na wala Hatowatazama Siku Ya Qiyaamah na wala Hatowatakasa na watapata adhabu iumizayo'. [Aal-'Imraan: 77]. [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy].
Hadiyth – 2
وعن أَبي أُمَامَة إياس بن ثعلبة الحارثي رضي الله عنه : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنِ اقْتَطَعَ حَقَّ امْرِىءٍ مُسْلِمٍ بِيَمِينِهِ ، فَقَدْ أَوْجَبَ اللهُ لَهُ النَّارَ . وَحَرَّمَ عَلَيْهِ الجَنَّةَ )) فَقَالَ لَهُ رَجُلٌ : وَإنْ كَانَ شَيْئاً يَسِيراً يَا رسولَ اللهِ ؟ قَالَ : (( وإنْ كَانَ قَضِيباً مِنْ أرَاكٍ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Umamah Iyaas bin Tha'labah Al-Haarithiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumnyang'anya mtu Muislamu haki yake kwa yamini la uwongo, imekuwa ni wajibu kwa Allaah kumuingiza motoni na kumharamishia Jannah." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن عبد اللهِ بن عمرو بن العاصِ رضي الله عنهما، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( الكَبَائِرُ : الإشْرَاكُ بِاللهِ ، وَعُقُوقُ الوَالِدَيْنِ ، وَقَتْلُ النَّفْسِ ، واليَمِينُ الغَمُوسُ )) . رواه البخاري .
وفي روايةٍ لَهُ : أنَّ أعْرابِياً جَاءَ إِلَى النبيّ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : يا رسولَ اللهِ مَا الكَبَائِرُ ؟ قَالَ : (( الإشْرَاكُ بِاللهِ )) قَالَ : ثُمَّ مَاذا ؟ قَالَ : (( اليَمِينُ الغَمُوسُ )) قلتُ : وَمَا اليَمِينُ الغَمُوسُ ؟ قَالَ : (( الَّذِي يَقْتَطِعُ مَالَ امْرِئٍ مُسْلِمٍ ! )) يعني بِيَمِينٍ هُوَ فِيهَا كَاذِبٌ .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Madhambi makubwa ni: Kumshirikisha Allaah, na kuwaasi wazazi wawili, na kuua nafsi na kula yamini la uwongo."[Al-Bukhaariy].
Na katika riwaayah yake nyengine: "Alikuja Mbedui kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akauliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Madhambi makubwa ni yepi?" Akasema: "Kumshirikisha Allaah." Akauliza tena: "Kisha ni gani?" Akasema: "Yamini la uwongo." Akasema: "Yamini la uwongo ni nini?" Akasema: "Ni ile ambayo kwayo hunyang'anywa Muislamu mali yake", yaani kwa yamini ambalo ndani yake yuwasema uwongo.