063-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Sunnah kwa Mwenye Kula Yamini Akaona Kufanya Kinyume na Yamini Hiyo Ndiyo Bora, Hivyo Alifanye Hilo Kisha Afanye Kafara la Kufanya Kinyume na Yamini Lake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب ندب من حلف عَلَى يَمينٍ فرأى غيرها خيراً مِنْهَا

أنْ يفعل ذَلِكَ المحلوف عَلَيْهِ ثُمَّ يُكَفِّر عن يمينه

063-Mlango Wa Sunnah kwa Mwenye Kula Yamini Akaona Kufanya Kinyume na Yamini Hiyo Ndiyo Bora, Hivyo Alifanye Hilo Kisha Afanye Kafara la Kufanya Kinyume na Yamini Lake

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن عبد الرحمان بن سَمُرَةَ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ لي رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( وَإِذَا حَلَفْتَ عَلَى يَمِينٍ ، فَرَأيْتَ غَيْرَهَا خَيْراً مِنْهَا ، فَأتِ الَّذِي هُوَ خَيرٌ وَكَفِّرْ عَنْ يَمِينِكَ )) . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abdir-Rahmaan bin Samurah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: "Na kama utakula yamini na akaona kisicho kuwa yamini yako ndicho bora basi fanya ambacho ni bora na itolee kafara yamini yako." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawud, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ حَلَفَ عَلَى يَمينٍ ، فَرَأى غَيْرَهَا خَيْراً مِنْهَا ، فَلْيُكَفِّرْ عَنْ يَمِينِهِ ، وَلْيَفْعَلِ الَّذِي هُوَ خَيْرٌ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Mwenye kula yamini na akaona kisicho kuwa yamini yako ndicho bora, aitolee kafara yamini na afanye ambacho ni bora." [Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي موسى رضي الله عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( إنِّي واللهِ إنْ شاءَ اللهُ لا أحْلِفُ عَلَى يَمِينٍ ، ثُمَّ أَرَى خَيراً مِنْهَا إِلاَّ كَفَّرْتُ عَنْ يَمِينِي ، وَأَتَيْتُ الَّذِي هُوَ خَيْرٌ )) . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Na mimi Wa-Allaahi! Allaah akitaka, sitakula yamini, halafu nikaona kinyume chake ni bora kuliko yamini hiyo isipokuwa nitaitolea kafara yamini yangu na nitakifanya ambacho ni bora zaidi." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة  رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( لأَنْ يَلَجَّ أَحَدُكُمْ في يَمِينِهِ في أهْلِهِ آثَمُ لَهُ عِنْدَ اللهِ تَعَالَى مِنْ أنْ يُعْطِي كَفَّارَتَهُ الَّتي فَرَضَ اللهُ عَلَيْهِ )) . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kuendelea mmoja wenu na yamini yake kwa jambo linalohusu familia yake, dhambi yake ni kubwa zaidi mbele ya Allaah kuliko kutoa kafara ambayo Allaah Ameiwajibisha juu yake." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share