069-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Kuitukana Homa
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كراهة سب الحمّى
069-Mlango Wa Ukaraha wa Kuitukana Homa
عن جابر رضي الله عنه : أنَّ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم دخلَ على أُمِّ السَّائِبِ ، أو أُمِّ المُسَيّبِ فَقَالَ : (( مَا لَكِ يَا أُمَّ السَّائِبِ – أو يَا أُمَّ المُسَيَّبِ – تُزَفْزِفِينَ ؟ )) قَالَتْ : الحُمَّى لاَ بَارَكَ اللهُ فِيهَا ! فَقَالَ : (( لاَ تَسُبِّي الحُمَّى فَإنَّهَا تُذْهِبُ خَطَايَا بَنِي آدَمَ كَمَا يُذْهِبُ الكِيْرُ خَبَثَ الحَدِيدِ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimzuru Ummus Saaib au Ummul Musayyab (Radhwiya Allaahu 'anhu), akamuuliza: "Una nini, ee Ummus Saaib au ee Ummus Musayyab? kwa nini unatetemeka?" Akasema: "Ni homa, Allaah Asiibariki." Akasema (Swalla Allaahu 'alyhi wa aalihi wa sallam): "Usiitukane homa, kawani inaondosha makosa ya mwanadamu kama vile tanuri (ya moto inayotumiwa na mfuaji vyuma) inavyosafisha uchafu wa chuma." [Muslim].