070-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kutukana Upepo na Kubainisha Kinacho Semwa Wakati wa Kuvuma Kwake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب النهي عن سب الريح ، وبيان ما يقال عند هبوبها 

070-Mlango Wa Kukatazwa Kutukana Upepo na Kubainisha Kinacho Semwa Wakati wa Kuvuma Kwake

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن أبي المنذِرِ أُبي بن كعب رضي الله عنه قال : قالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تَسُبُّوا الرِّيحَ ، فَإِذَا رَأَيْتُمْ مَا تَكْرَهُونَ ، فَقُولُوا : اللَّهُمَّ إنَّا نَسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ هذِهِ الرِّيحِ وَخَيْرِ مَا فِيهَا وخَيْرِ مَا أُمِرَتْ بِهِ . وَنَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ هذِهِ الرِّيحِ وَشَرِّ مَا فِيهَا وَشَرِّ مَا أُمِرَتْ بِهِ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Mundhir Ubayy bin Ka'ab (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Usiutukane upepo, mukiona munayo yachukia, semeni: 'Allaahumma inniy nasaluka min khayri haadhihir riyh wa khayri maa fiyhaa wa khayri maa umirat bihi wa na'uwdhu bika min sharri haadhihir riyh wa sharri maa umirat bihi (Ee Rabb wangu! Hakika sisi tunakuomba kheri ya upepo huu na kheri iliyo ndani yake na kheri kilicho amrishwa kwayo. Na tunajilinda Kwako na shari ya upepo huu na shari iliyoko ndani yake na shari kilicho amrishwa kwayo)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh].

 

Hadiyth – 2

وعن أبي هريرة رضي الله عنه قال : سمعتُ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( الرِّيحُ مِنْ رَوحِ اللهِ ، تَأتِي بِالرَّحْمَةِ ، وَتَأتِي بِالعَذَابِ ، فَإذَا رَأَيْتُمُوهَا فَلاَ تَسُبُّوهَا ، وَسَلُوا اللهَ خَيْرَهَا ، وَاسْتَعِيذُوا باللهِ مِنْ شَرِّهَا )) . رواه أبو داود بإسناد حسن .

Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Upepo ni baraka kutoka kwa Allaah, unakuja pamoja na rehema na adhabu. Hivyo, mnapouona musiutukane na mtakeni Allaah Awapatieni kheri kutoka kwa huo upepo na takeni ulinzi kwa Allaah kutokana na shari yake (huo upepo)." [Abu aawuwd kwa Isnaad iliyo Hasan]

 

Hadiyth – 3

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كان النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم إذا عَصَفَتِ الرِّيحُ قال : (( اللَّهُمَّ إنِّي أسْألُكَ خَيْرَهَا وَخَيْرَ مَا فِيهَا وَخَيْرَ مَا أُرْسِلَتْ بِهِ ، وأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّهَا وَشَرِّ مَا فِيهَا وَشَرِّ مَا أُرْسِلَتْ بِهِ )) . رواه مسلم .

Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) unapovuma upepo wa nguvu akiomba: "Allaahumma inniy asaluka khayrahaa wa khayra maa fiyhaa wa khayra maa ursilat bihi wa a'uwdhu bika min sharrihaa wa sharri maa fiyhaa wa sharri maa ursilat bihi (Ee Rabb wangu! Hakika mimi ninakuomba kheri yake na kheri iliyo ndani yake na kheri kilicho amrishwa kwayo. Na ninajilinda Kwako na shari ya upepo huu na shari iliyoko ndani yake na shari kilicho amrishwa kwayo)." [Muslim]

 

 

Share