072-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa kwa Mtu Kusema: Tumepata Mvua Kutokana na Nyota Kadha
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن قول الإنسان : مُطِرنا بنَوء كذا
072-Mlango Wa Kukatazwa kwa Mtu Kusema: Tumepata Mvua Kutokana na Nyota Kadha
عن زيد بن خالد رضي الله عنه قال : صلَّى بنا رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم صَلاَةَ الصُّبْحِ بِالحُدَيْبِيَّةِ في إثْرِ سَمَاءٍ كَانَتْ مِنَ اللَّيْلِ ، فَلَمَّا انْصَرَفَ أقْبَلَ عَلَى النَّاسِ ، فقالَ : (( هَلْ تَدْرُونَ مَاذَا قالَ رَبُّكُمْ ؟ )) قالُوا : اللهُ وَرَسُولُهُ أعْلَمُ . قال : (( قالَ : أصْبَحَ مِنْ عِبَادِي مُؤْمِنٌ بِي ، وَكَافِرٌ ، فَأَمَّا مَنْ قَالَ : مُطِرْنَا بِفَضْلِ اللهِ وَرَحْمَتِهِ ، فَذلِكَ مُؤْمِنٌ بِي كَافِرٌ بِالكَوْكَبِ ، وأَما مَنْ قَالَ مُطِرْنَا بِنَوءِ كَذَا وَكَذَا ، فَذلكَ كَافِرٌ بِي مُؤْمِنٌ بِالكَوْكَبِ )) . متفق عليه .
Amesema Zayd bin Khaalid (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alituswalisha sisi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Swalaah ya Asubuhi katika Hudaybiyah baada ya mvuaa zilizonyesha usiku uliopita. Alipomaliza akawaelekea watu na kuwauliza: "Je, mnaelewa Alichosema Rabb wenu?" Wakajibu: "Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi." Akasema: "Baadhi ya waja wangu wamepambazukiwa na asubuhi wakiwa Wananiamini na baadhi Wamenikufuru; ama aliyesema tumepata mvua kwa fadhila ya Allaah na Rehema Zake, basi huyo ni mwenye kuniamini na mwenye kukufuru nyota; ama mwenye kusema tumepata mvua kutokana na nyota kadha wa kadha huyo Amenikufuru na ni mwenye kuamini nyota." [Al-Bukhaariy na Muslim]