073-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Kumwambia Muislamu: Ee Kafiri
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تحريم قوله لمسلم : يا كافر
073-Mlango Wa Uharamu wa Kumwambia Muislamu: Ee Kafiri
Hadiyth – 1
عن ابن عمر رضي الله عنهما ، قال : قالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( إذَا قَالَ الرَّجُلُ لأَخِيهِ : يَا كَافِرُ ، فَقَدْ بَاءَ بِهَا أَحَدُهُمَا ، فَإنْ كانَ كَمَا قَالَ وَإلاَّ رَجَعَتْ عَلَيْهِ )) متفق عليه .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapomwambia mtu ndugu yake, ee kafiri! Basi hakika (ukafiri huo utakuwa) umethibiti kati ya mmoja wao. Ikiwa ni kama alivyosema (aliyeitwa hivyo atakuwa kama alivyoambiwa kafiri) na ikiwa ni kinyume na hivyo ukafiri utarudi kwake (yaani msemaji)." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أبي ذرٍّ رضي الله عنه : أنَّه سَمِعَ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقولُ : (( مَنْ دَعَا رَجُلاً بالكُفْرِ ، أو قالَ : عَدُوَّ اللهِ ، وَلَيْسَ كَذلكَ إلاَّ حَارَ عَلَيْهِ )) . متفق عليه .
Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mwenye kumuita mtu mwengine kafiri au akasema: adui wa Allaah na si kama alivyosema isipokuwa sifa hiyo hurudi kwake." [Al-Bukhaariy na Muslim]