074-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kutoa Maneno Machafu na ya Kishenzi

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب النهي عن الفحش وبذاء اللسان

074-Mlango Wa Kukatazwa Kutoa Maneno Machafu na ya Kishenzi

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن ابن مسعودٍ رضي الله عنه ، قال : قالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( لَيْسَ المُؤْمِنُ بالطَّعَّانِ ، وَلاَ اللَّعَّانِ ، وَلاَ الفَاحِشِ ، وَلاَ البَذِيِّ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Muumini hawi ni mwenye kusuta wala kulaani kutupa maneno machafu wala kutusi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 2

وعن أنسٍ رضي الله عنه قال : قالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( مَا كَانَ الفُحْشُ فِي شَيْءٍ إلاَّ شَانَهُ ، وَمَا كَانَ الحَيَاءُ فِي شَيْءٍ إلاَّ زَانَهُ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Utumiaji wa maneno machafu hauchang'anyiki na kitu chochote isipokuwa hukichafua. Na haya haiwi pamoja na kitu chochote isipokuwa hukirembehsa." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Share