075-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Mazungumzo ya Kukera na kuvupa Mipaka Ndani Yake na Kujikalifisha katika Ufasaha na Kutumia Lugha Mbaya
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كراهة التقعير في الكلام
والتشدُّق فيه وتكلف الفصاحة واستعمال وحشي اللُّغة
ودقائق الإعراب في مخاطبة العوام ونحوهم
075-Mlango Wa Ukaraha wa Mazungumzo ya Kukera na kuvupa Mipaka Ndani Yake na Kujikalifisha katika Ufasaha na Kutumia Lugha Mbaya
Hadiyth – 1
عن ابن مسعود رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قال : (( هَلَكَ المُتَنَطِّعُونَ )) قَالَهَا ثَلاَثاً . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wameangamia wenye kushadidisha mambo." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما : أنَّ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال : (( إنَّ اللهَ يُبْغِضُ البَلِيغَ مِنَ الرِّجَالِ الَّذي يَتَخَلَّلُ بِلِسَانِهِ كَمَا تَتَخَلَّلُ البَقَرَةُ )) . رواه أبو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah Anamchukia mwenye kugeuza ulimi wake kwa ufasaha wa mazungumzo miongoni mwa wanaume sawa na vile anavyofanya ng'ome anapokuwa kala malisho yake." [Abu Daawud na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 3
وعن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قال : (( إنَّ مِنْ أحَبِّكُمْ إِلَيَّ ، وأقْرَبِكُمْ مِنِّي مَجْلِساً يَومَ القِيَامَةِ ، أحَاسِنكُمْ أَخْلاَقَاً ، وإنَّ أَبْغَضَكُمْ إلَيَّ ، وأبْعَدَكُمْ مِنِّي يَومَ القِيَامَةِ ، الثَّرْثَارُونَ وَالمُتَشَدِّقُونَ وَالمُتَفَيْهِقُونَ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) . وقد سبق شرحه في بَابِ حُسْنِ الخُلُقِ .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir bin 'Abdillaah (radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika watakaopendwa zaidi na watakao kuwa karibu nami Siku ya Qiyaamah ni wale wenye tabia nzuri. Na hakika nitakaowachukia na watakao kuwa mbali nami Siku ya Qiyaamah ni wale ma-tharthar (wale wenye kuzungumza sana kwa kujikalifisha) na mutashaddiquwn (wanaorefusha mazungumzo yao kwa watu na waazungumza kwa kujaza midomo yaokwa majisifu) na mutafayhiquwn (Wenye kiburi)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]