077-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Kuziita Zabibu kwa Jina Karm
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كراهة تسمية العنب كرماً
077-Mlango Wa Ukaraha wa Kuziita Zabibu kwa Jina Karm
Hadiyth – 1
عن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تُسَمُّوا العِنَبَ الكَرْمَ ، فَإنَّ الكَرْمَ المُسْلِمُ )) متفق عليه ، وهذا لفظ مسلم .
وفي رواية : (( فَإنَّمَا الكَرْمُ قَلْبُ المُؤمِنِ )) . وفي رواية للبخاري ومسلم :
(( يَقُولُونَ الكَرْمُ ، إنَّمَا الكَرْمُ قَلْبُ المُؤْمِنِ )) .
Imepoewa kutoka kwake Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msiite zabibu Karm, hakika Al-Karm ni Muislamu." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya Muslim].
Na katika riwaayah nyengine: "Kwa hakika si kitu kingine bali Al-Karm ni moyo wa Muumini."
Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy na Muslim: "Watu husema: 'Al-Karm (ukarimu).' Hakika si kitu kingine bali Al-Karm ni moyo wa Muumini."
Hadiyth – 2
وعن وائلِ بنِ حُجرٍ رضي الله عنه ، عن النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قال : (( لاَ تَقُولُوا : الكَرْمُ ، وَلكِنْ قُولُوا : العِنَبُ ، والحَبَلَةُ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Waail bin Hujr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Musiseme: 'Al-Karam', lakini semeni: 'Al-'inab (zabibu) na Al-Habalah (zabibu)'." [Muslim]