088-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Kugeuka Geuka katika Swalaah Bila Udhuru Wowote
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كراهة الالتفات في الصلاة لغير عذر
088-Mlango Wa Ukaraha wa Kugeuka Geuka katika Swalaah Bila Udhuru Wowote
Hadiyth – 1
عن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها ، قالت : سألت رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم عَنِ الالتفَاتِ في الصَّلاَةِ ، فَقَالَ : (( هُوَ اخْتِلاَسٌ يَخْتَلِسُهُ الشَّيْطَانُ مِنْ صَلاَةِ العَبْدِ )) . رواه البخاري .
Amasema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu kugeuka (upande wa kulia na kushoto) katika Swalaah, akasema: "Kufanya hivyo ni udokozi anaodokoa shetani katika Swalaah ya mja." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 2
وعن أنس رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( إيَّاكَ والالتِفَاتَ فِي الصَّلاَةِ ، فَإنَّ الالتفَاتَ في الصَّلاَةِ هَلَكَةٌ ، فَإنْ كَانَ لاَ بُدَّ ، فَفِي التَّطَوُّعِ لاَ في الفَريضَةِ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: "Jiepushe na kugeuka geuka katika Swalaah, kwani kugeuka katika Swalaah ni maangamivu. Ikiwa hapana budi mpaka ugeuke basi iwe sio katika Swalaah ya faradhi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]