087-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kunyanyua Macho Juu Mbinguni katika Swalaah
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن رفع البصر إِلَى السماء في الصلاة
087-Mlango Wa Kukatazwa Kunyanyua Macho Juu Mbinguni katika Swalaah
عن أنس بن مالك رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( مَا بَالُ أقْوامٍ يَرْفَعُونَ أبْصَارَهُمْ إِلَى السَّمَاءِ في صَلاَتِهِمْ ! )) فَاشْتَدَّ قَولُهُ في ذَلِكَ حَتَّى قَالَ :(( لَيَنْتَهُنَّ عَنْ ذَلِكَ ، أَوْ لَتُخطفَنَّ أَبْصَارُهُمْ ! )) . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wana nini watu wanaonyanyua macho yao juu mbinguni wakiwa katika Swalaah zao." Akawa mkali na kuwaonya wasifanye hivyo mpaka akasema: "Wakome kufanya hivyo au watapofolewa macho yao." [Al-Bukhaariy]