086-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Kuswali Pindi Chakula Kinapokuwa Tayari na Nafsi yake Imevutiwa Kwayo au Kushikwa na Haja Mbili: Nazo ni Ndogo na Kubwa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب كراهة الصلاة بحضرة الطعام ونفسه تتوق إِلَيْهِ

أَوْ مَعَ مدافعة الأخبثين : وهما البول والغائط

086-Mlango Wa Ukaraha wa Kuswali Pindi Chakula Kinapokuwa Tayari na Nafsi yake Imevutiwa Kwayo au Kushikwa na Haja Mbili: Nazo ni Ndogo na Kubwa

 

Alhidaaya.com

 

عن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها ، قالت : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( لا صَلاَةَ بِحَضْرَةِ طَعَامٍ ، وَلاَ وَهُوَ يُدَافِعُهُ الأَخْبَثَانِ )) . رواه مسلم .

Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hapana Swalaah pindi chakula kinapokuwa tayari wala anapotingwa na uchafu wa aina mbili (yaani haja ndogo na kubwa)." [Muslim]

 

 

Share