096-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uzito wa Uharamu wa Mtumwa Kutoroka Kutoka kwa Bwana Wake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب تغليظ تحريم إباق العبد من سيده

096-Mlango Wa Uzito wa Uharamu wa Mtumwa Kutoroka Kutoka kwa Bwana Wake

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن جرير رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( أَيُّمَا عَبْدٍ أَبَقَ ، فَقَدْ بَرِئَتْ مِنْهُ الذِّمَّةُ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Jariyr bin 'Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtumwa yeyote anayekimbia (kutoka kwa bwana wake), hakika anakosa (na kuwa mbali) ulinzi wa Uislamu aliopatiwa." [Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن جرير رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا أَبَقَ العَبْدُ ، لَمْ تُقْبَلْ لَهُ صَلاَةٌ )) . رواه مسلم .

وفي روايةٍ : (( فَقَدْ كَفَرَ )) .

Imepokewa kutoka kwa Jariyr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Pindi anapotoroka mtumwa (kutoka kwa bwana wake), Swalaah yake haitakubaliwa." [Muslim]

Na katika riwaayah nyengine: "Hakika amekufuru."

 

Share