106-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Kurudisha Zawadi ya Manukato Bila Udhuru
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كراهة رد الريحان لغير عذر
106-Mlango Wa Ukaraha wa Kurudisha Zawadi ya Manukato Bila Udhuru
Hadiyth – 1
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ عُرِضَ عَلَيْهِ رَيْحَانٌ ، فَلاَ يَرُدَّهُ ، فَإنَّهُ خَفيفُ المَحْمِلِ ، طَيِّبُ الرِّيحِ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kupatiwa zawadi ya manukato asirudishe, kwani ni nyepesi kubebwa na yenye harufu nzuri." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أنس بن مالكٍ رضي الله عنه : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ لاَ يَرُدُّ الطِّيبَ . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa ni mwenye kurudisha zawadi ya manukato. [Al-Bukhaariy]