105-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa kutoka Msikitini Baada ya Adhana Isipokuwa kwa Udhuru Mpaka Aswali Swalaah ya Faradhi
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كراهة الخروج من المسجد بعد الأذان
إلا لعذر حتى يصلي المكتوبة
105-Mlango Wa Ukaraha wa kutoka Msikitini Baada ya Adhana Isipokuwa kwa Udhuru Mpaka Aswali Swalaah ya Faradhi
عن أبي الشَّعْثَاءِ ، قالَ : كُنَّا قُعُوداً مَع أبي هريرة رضي الله عنه في المَسْجِدِ ، فَأَذَّن المُؤَذِّنُ ، فَقَامَ رَجُلٌ مِنَ المَسْجِدِ يَمْشِي ، فَأَتْبَعَهُ أبُو هُريرَةَ بَصَرَهُ حَتَّى خَرَجَ مِنَ المَسْجِدِ ، فقال أبو هريرة : أمَّا هذَا فَقَدْ عَصَى أبا القَاسِمِ صلى الله عليه وسلم . رواه مسلم .
Amesema Abu Ash-Sha'athaa: Tulikuwa tumekaa pamoja na Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Msikitini, mara muadhini akaadhini. Hapo akasimama mtu mmoja akawa anatembea (kutaka kutoka nje ya Msikiti). Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) akamfuata kwa kumwangalia mpaka akatoka Msikitini. Hapo, Abu Huraiyrah akasema: "Ama mtu huyu hakika amemuasi Abul Qaasim (yaani Muhammad Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). [Muslim]