104-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kumuashiria muislamu kwa Silaha na Mfano wake Sawa ni kwa Kweli au Mzaha na Katazo la Kuwa na Upanga Nje ya Ala yake
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن الإشارة إلى مسلم بسلاح ونحوه
سواء كان جاداً أو مازحاً ، والنهي عن تعاطي السيف مسلولاً
104-Mlango Wa Kukatazwa Kumuashiria muislamu kwa Silaha na Mfano wake Sawa ni kwa Kweli au Mzaha na Katazo la Kuwa na Upanga Nje ya Ala yake
Hadiyth – 1
عن أبي هريرة رضي الله عنه ، عن رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال : (( لاَ يُشِرْ أحَدُكُمْ إلَى أخِيهِ بِالسِّلاحِ ، فَإنَّهُ لاَ يَدْرِي لَعَلَّ الشَّيْطَانَ يَنْزعُ فِي يَدِهِ ، فَيَقَع فِي حُفْرَةٍ مِنَ النَّارِ )) . متفق عليه .
وفي رواية لمسلم قال : قال أبو القاسم صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ أشَارَ إلَى أخِيهِ بِحَدِيدَةٍ ، فَإنَّ المَلاَئِكَةَ تَلْعَنُهُ حَتَّى يَنْزعَ ، وَإنْ كَانَ أخَاهُ لأَبِيهِ وَأُمِّهِ ))
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Asimuashirie mmoja wenu nduguye kwa silaha, kwani yeye hajui huenda shetani akaitowa mkononi mwake (akaleta maafa, kujeruhi, au kifo), hivyo kumfanya aingie katika shimo la moto." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na Musli katika riwaayah yake amesema: Amesema Abul Qaasim: "Mwenye kumuashiria chuma nduguye, hakika Malaaikah anamlaani mpaka akiondoshe, japokuwa atakuwa ni ndugu yake halisa (kwa baba na mama)."
Hadiyth – 2
وعن جابر رضي الله عنه قال : نهى رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم أنْ يُتَعَاطَى السَّيْفُ مَسْلُولاً . رواه أبو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Amesema Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu): Amekataza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mtu kumpatia upanga usiokuwa katika ala yake mwenziwe. [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]