103-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kufuja Mali kwa Njia Ambayo Haikuidhinishwa na Sheria
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن إضاعة المال في غير وجوهه
التي أذن الشرع فيها
103-Mlango Wa Kukatazwa Kufuja Mali kwa Njia Ambayo Haikuidhinishwa na Sheria
Hadiyth – 1
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ اللهَ تعالى يَرْضَى لَكُمْ ثَلاَثاً ، ويَكْرَهُ لَكُمْ ثَلاَثاً : فَيَرْضَى لَكُمْ أنْ تَعْبُدُوهُ ، وَلاَ تُشْرِكُوا بِهِ شَيئاً ، وَأَنْ تَعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللهِ جَمِيعاً وَلاَ تَفَرَّقُوا ، وَيَكْرَهُ لَكُمْ : قِيلَ وَقَالَ ، وَكَثْرَةَ السُّؤَالِ ، وإضَاعَةَ المَالِ )) . رواه مسلم
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah Ta'aalaa Anawaridhia mambo matatu na Anachukia mambo matatu kwenu: Anawaridhia muwe ni wenye kumuabudu Yeye wala usimshirikishe na chochote, na mushikamane na kamba ya Allaah wala musifarikiane. Na Anachukia kwenu nyinyi: Uvumi (na kuzungumza sana mazungumzo yasiyo na faida), na kuuliza maswali mengi na kufuja mali." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن ورَّادٍ كاتب المغيرة، قال : أَمْلَى عَلَيَّ المُغِيرَةُ بْنُ شُعْبَةَ في كِتابٍ إلَى مُعَاوِيَةَ رضي الله عنه : أنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَقُولُ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلاَةٍ مَكْتُوبَةٍ : (( لاَ إلهَ إلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لهُ ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ، اللَّهُمَّ لاَ مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ ، وَلاَ مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ ، وَلاَ يَنْفَعُ ذَا الجَدِّ مِنْكَ الجَدُّ )) وَكَتَبَ إلَيْهِ أَنَّهُ كَانَ يَنْهَى عَنْ قِيلَ وَقَالَ ، وَإضَاعَةِ المَالِ ، وَكَثْرَةِ السُّؤَالِ ، وَكَانَ يَنْهَى عَنْ عُقُوقِ الأُمَّهَاتِ ، وَوَأْدِ البَنَاتِ ، وَمَنْعٍ وَهَاتِ . متفق عليه
Amesema Warraad, mwandishi wa Mughiyrah bin Shu'bah (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Mughiyrah bin Shu'bah (Radhwiya Allaahu 'anhu) alinifanya imla ya baruwa kwenda kwa Mu'awiyah, kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anasema baada ya kila Swalaah ya faradhi: "Laa ilaaha illa Allaah wahdahu laa shariyka lahu, lahul Mulku wa lahul Hamdu wa Huwa 'alaa kuli shayyin Qadiyr, Allaahumma laa maani'a lima a'twayta wa laa Mu'twiya lima mana'ta wa laa yanfa'u dhal jaddi minkal jadd (Hakuna mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allaah Peke Yake Hana mshirika, mwenye Ufalme na Mwenye kila Sifa Nzuri, Naye ni Muweza wa kila kitu. Ee Rabb Wangu! Hakuna wa kuzuia Ulichokitoa; na wala hakuna anayekitoa Unachokizuia; na wala hautamfaa Kwako mwenye utajiri wake)." Na pia akamwandikia kwamba: "Alikuwa (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anakataza maneno ya kipuuzi, na kufuja mali na kuuliza maswali mengi. Na pia (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alikataza kuwaasi akina mama, na kuwazika wasichana wakiwa hai na kumpokonya (kumchukulia) mtu haki yake." [Al-Bukhaariy na Muslim]