102-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu kwa Mtu wa Mjini Kununua kwa Mtu wa Kijijini na Kupokea Njiani Msafara wa Wafanya Biashara, na Kuuza katika Mauzo ya Nduguye, na Posa Juu ya Posa yake Isipokuwa Akitoa Ruhusa au Akikataliwa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب تحريم بيع الحاضر للبادي وتلقي الركبان

والبيع على بيع أخيه والخِطبة على خطبته إلا أنْ يأذن أو يردّ

102-Mlango Wa Uharamu kwa Mtu wa Mjini Kununua kwa Mtu wa Kijijini na Kupokea Njiani Msafara wa Wafanya Biashara, na Kuuza katika Mauzo ya Nduguye, na Posa Juu ya Posa yake Isipokuwa Akitoa Ruhusa au Akikataliwa

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن أنس رضي الله عنه ، قالَ : نهَى رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم أنْ يَبيعَ حَاضِرٌ لِبَادٍ وإنْ كانَ أخَاهُ لأَبِيهِ وَأُمِّهِ . متفق عليه .

Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Amekataza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) watu wa mjini kuuza bidhaa za aliyetoka mshambani hata akiwa za kaka yake, baba na mama yake. [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قال : قالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تَتَلَقَّوُا السِّلَعَ حَتَّى يُهْبَطَ بِهَا إلَى الأَسْوَاقِ )) . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msipokee wafanaya biashara kwa kununua bidhaa kutoka kwao kwa kukutana nao njiani kabla haujafika sokoni." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قال : قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تَتَلَقَّوُا الرُّكْبَانَ ، وَلاَ يَبِعْ حَاضِرٌ لِبَادٍ )) فقالَ لَهُ طَاووسٌ : مَا : لاَ يَبيعُ حَاضِرٌ لِبَادٍ ؟ قال : لاَ يَكُونُ لَهُ سِمْسَاراً . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msiende kuupokea njiani msafara wa wafanya biashara na wala mtu wa mjini (kwa kujifanya dalali) asiuze bidhaa ya aliyetoka shamba." Akamuuliza yeye Twaa'uws: "Nini maana ya wa mjini asiuze mali ya mtu wa kijijini (shamba)?" Akamjibu: "Asiwe dalali." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن أبي هريرة رضي الله عنه قال : نَهَى رسولُ الله صلى الله عليه وسلم أنْ يَبِيعَ حَاضِرٌ لِبَادٍ ، وَلاَ تَنَاجَشُوا وَلاَ يَبِيع الرَّجُلُ عَلَى بَيْعِ أخْيِهِ ، وَلاَ يَخْطُبُ عَلَى خِطْبَةِ أخِيهِ ، وَلاَ تَسْأَلُ المَرْأَةُ طَلاَقَ أُخْتِهَا لِتَكْفَأَ مَا فِي إنائِهَا .

وفي رواية قال : نَهَى رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم عَنِ التَّلَقِّي، وَأَنْ يَبْتَاعَ المُهَاجِرُ لِلأعْرَابِيِّ ، وَأَنْ تَشْتَرِطَ المَرْأةُ طَلاَقَ أُخْتِهَا ، وأنْ يَسْتَامَ الرَّجُلُ على سَوْمِ أخِيهِ ، وَنَهَى عَنِ النَّجْشِ والتَّصْرِيَةِ . متفق عليه .

Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Amekataza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mtu wa mjini kuuza bidhaa za mtu aliyetoka kijijini wala msihadaiane wala mtu asiuze katikamauzo ya nduguye wala asipose mmoja wenu juu ya posa ya nduguye, wala mwanamke asitake dada yake aachwe ili aolewe yeye na achukue sehemu yake. 

Na katika riwaayah nyengine: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kupokea bidhaa njiani, na amekataza mtu mjini kuuza bidhaa za mtu wa shamba, na mwanamke kuolewa kwa sharti la kuachwa mwenzake. Na mtu kununua au kutaka maafikiani ya kibiashara ya ndugu yake na amekataza ulaghai wa ndani na kuacha kumkama mnyama ili kumhadaa mnunuzi." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 5

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم قال : (( لاَ يَبِعْ بَعْضُكُمْ عَلَى بَيْعِ بَعْضٍ ، وَلاَ يَخْطُبْ عَلَى خِطْبَةِ أخِيهِ إلاَّ أنْ يَأذَنَ لَهُ )) . متفق عليه ، وهذا لفظ مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Ibnm 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wala baadhi yenu wasiuze katika mauzo ya baadhi ya wengine wala asipose mmoja wenu juu ya posa ya nduguye isipokuwa anapompatia idhini." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hili ni tamshi la Muslim]

 

Hadiyth – 6

وعن عقبة بن عامر رضي الله عنه : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم قال : (( المُؤْمِنُ أَخُو المُؤْمِنِ ، فَلاَ يَحِلُّ لِمُؤْمِنٍ أنْ يَبْتَاعَ عَلَى بَيْعِ أخِيهِ وَلاَ يَخْطُبَ عَلَى خِطْبَةِ أخِيهِ حَتَّى يذَرَ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa "Uqbah bin 'Aamir kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Muumini ni ndugu yake Muumini mwengine, hivyo si halali kwa Muumini kuuza katika mauzo ya nduguye wala asipose juu ya posa ya nduguye mpaka ajitoe (kwa kutotaka kumuoa huyo mwanamke)." [Muslim]

 

 

 

 

Share