101-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Mwanamke Kukaa na Msiba wa Maiti Zaidi ya Siku Tatu Isipokuwa kwa Mumewe Ambao ni Miezi Minne na Siku Kumi
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تحريم إحداد المرأة على ميت فوق ثلاثة أيام
إلا على زوجها أربعة أشهر وعشرة أيام
101-Mlango Wa Uharamu wa Mwanamke Kukaa na Msiba wa Maiti Zaidi ya Siku Tatu Isipokuwa kwa Mumewe Ambao ni Miezi Minne na Siku Kumi
عن زينب بنتِ أبي سلمة رضي الله عنهما ، قالت : دَخَلْتُ عَلَى أُمِّ حَبِيبَةَ رضيَ اللهُ عنها ، زَوجِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ، حِينَ تُوُفِّيَ أبُوهَا أبُو سُفْيَانَ بن حرب رضي الله عنه ، فَدَعَتْ بِطِيبٍ فِيهِ صُفْرَةُ خَلُوقٍ أوْ غَيرِهِ ، فَدَهَنَتْ مِنهُ جَارِيَةً ، ثُمَّ مَسَّتْ بِعَارِضَيْهَا ، ثُمَّ قَالَتْ : واللهِ مَا لِي بِالطِّيبِ مِنْ حَاجَةٍ ، غَيْرَ أنِّي سَمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقُولُ عَلَى المِنْبَرِ : (( لا يَحِلُّ لامْرَأَةٍ تُؤْمِنُ بِاللهِ وَاليَوْمِ الآخِرِ أنْ تُحِدَّ على مَيِّتٍ فَوقَ ثَلاَثِ لَيَالٍ ، إلاَّ علَى زَوْجٍ أرْبَعَةَ أشْهُرٍ وَعَشْراً )) .
قالَتْ زَيْنَبُ : ثُمَّ دَخَلْتُ عَلَى زَيْنَبَ بنْتِ جَحْشٍ رضي اللهُ عنها حينَ تُوُفِّيَ أَخُوهَا ، فَدَعَتْ بِطِيبٍ فَمَسَّتْ مِنْهُ ثُمَّ قَالَتْ : أمَا وَاللهِ مَا لِي بِالطِّيبِ مِنْ حَاجَةٍ ، غَيرَ أنِّي سَمِعْتُ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقُولُ عَلَى المِنْبَرِ : (( لا يَحِلُّ لامْرَأَةٍ تُؤْمِنُ بِاللهِ وَاليَوْمِ الآخِرِ أنْ تُحِدَّ على مَيِّتٍ فَوقَ ثَلاَثٍ، إلاَّ علَى زَوْجٍ أرْبَعَةَ أشْهُرٍ وَعَشْراً )). متفق عليه .
Amesema Zaynab Bint Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Niliingia kwa Umm Habibah (Radhwiya Allaahu 'anhaa), mke wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipofariki baba yake Abu Sufyaan bin Harb (Radhwiya Allaahu 'anhu), akataka (yaani Umm Habibah) aletewe manukato ndani yake mna sufrah, Khaluq au mwengine akampaka baadhi yake kijakazi, kisha akapaka mashavuni mwake, kisha akasema: "Wa-Allaahi, sina haja ya manukato isipokuwa mimi nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya minbar akisema: 'Haifai kwa mwanamke anayemuamini Allaah na Siku ya Mwisho kukaa msiba kwa sababu ya maiti zaidi ya siku tatu isipokuwa kwa mume wake kwa muda wa miezi minne na siku kumi'." Akasema Zaynab: Kisha nikaingia kwa Zaynab bint Jahsh (Radhwiya Allaahu 'anhaa) alipofariki kaka yake, akataka aletewe manukato, akapata kidogo, kisha akasema: "Ama Wa-Allaahi, sina haja ya manukato isipokuwa mimi nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya mimbar akisema: 'Haifai kwa mwanamke anayemuamini Allaah na Siku ya Mwisho kukaa msiba kwa sababu ya maiti zaidi ya siku tatu isipokuwa kwa mume wake kwa muda wa miezi minne na siku kumi'." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy].