100-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Mzazi Kuwapendelea Baadhi ya Watoto Wake Juu ya Wengine Katika Hiba
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كراهة تفضيل الوالد بعض أولاده
على بعض في الهبة
100-Mlango Wa Ukaraha wa Mzazi Kuwapendelea Baadhi ya Watoto Wake Juu ya Wengine Katika Hiba
عن النعمان بن بشير رضي الله عنهما : أنَّ أباه أتَى بِهِ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم فقال : إنِّي نَحَلْتُ ابْنِي هَذَا غُلاماً كَانَ لِي ، فقال رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( أكُلَّ وَلَدِكَ نَحَلْتَهُ مِثْلَ هَذَا ؟ )) فقال : لا ، فقالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( فَأرْجِعهُ )) .
وفي روايةٍ: فقال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( أَفَعَلْتَ هذَا بِوَلَدِكَ كُلِّهِمْ ؟ )) قال : لا ، قال : (( اتَّقُوا الله واعْدِلُوا فِي أوْلادِكُمْ )) فَرَجَعَ أبي ، فَرَدَّ تِلْكَ الصَّدَقَةَ .
وفي روايةٍ : فقال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( يَا بَشيرُ ألَكَ وَلَدٌ سِوَى هَذَا ؟ )) فقالَ : نَعَمْ ، قال : (( أكُلَّهُمْ وَهَبْتَ لَهُ مِثْلَ هذَا ؟ )) قال : لا ، قال : (( فَلاَ تُشْهِدْنِي إذاً فَإنِّي لاَ أشْهَدُ عَلَى جَوْرٍ )) .
وفي روايةٍ : (( لاَ تُشْهِدْنِي عَلَى جَوْرٍ )) .
وفي رواية : (( أشْهِدْ عَلَى هذَا غَيْرِي ! )) ثُمَّ قال : (( أيَسُرُّكَ أنْ يَكُونُوا إلَيْكَ في البِرِّ سَواءً ؟ )) قال : بَلَى ، قال : (( فَلا إذاً )) . متفق عليه .
Imepokewa kutoka kwa An-Nu'maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa, baba yake alimpeleka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Hakika nimempa mtumwa mwanangu huyu." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza: "Watoto wako wote umewapa kama hivyo?" Akajibu: "Hapana." Akamwambia: "Basi mrudishe."
Na katika riwaayah nyengine: Akasema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Umefanya hivyo kwa watoto wako wote?" Akajibu: "Hapana." Akasema: "Mcheni Allaah na mfanye uadilifu kati ya watoto wenu." Alirudi babangu na kurejesha zawadi hiyo.
Na katika riwaayah nyengine: Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ee Bashiyr! Je, una watoto wengine mbali na huyu?" Akajibu: "Ndio." Akasema: "Je, umewapatia wote mfano wa huyu?" Akajibu: "Hapana." Akasema: "Hivyo, usinifanye mimi kuwa shahidi kwani mimi siwi shahidi wa udhalimu."
Na katika riwaayah nyengine: "Usinifanye shahidi kwa udhalimu."
Na katika riwaayah nyengine: "Mfanye asiyekuwa mimi kuwa shahidi." Kisha akasema: "Je, unapenda watoto wako wakutendee wema sawasawa." Akajibu: "Ndio." Akasema: "Hivyo, usifanye udhalimu sasa." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy].