117-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Anachosema wa Anachofanya Mwenye Kufanya Alichokatazwa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب ما يقوله ويفعله من ارتكب منهياً عنه

117-Mlango Wa Anachosema wa Anachofanya Mwenye Kufanya Alichokatazwa

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۖ ﴿٣٦﴾

Na utakapokuchochea uchochezi kutoka kwa shaytwaan, basi omba kinga kwa Allaah. [Fusw-swilat: 41]

إِنَّ الَّذِينَ اتَّقَوْا إِذَا مَسَّهُمْ طَائِفٌ مِّنَ الشَّيْطَانِ تَذَكَّرُوا فَإِذَا هُم مُّبْصِرُونَ ﴿٢٠١﴾

Hakika wale wenye taqwa zinapowagusa pepesi za shaytwaan hukumbuka, basi mara wao huwa wenye kuona kwa utambuzi. [Al-A'raaf: 201]

وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٣٥﴾

Na ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao (kwa maasi), humdhukuru Allaah wakaomba Maghfirah kwa madhambi yao. Na nani anayeghufuria madhambi isipokuwa Allaah. Na hawaendelei katika waliyoyafanya na hali wanajua.

أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُم مَّغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَجَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿١٣٦﴾

Hao jazaa yao ni Maghfirah kutoka kwa Rabb wao na Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo. Ni uzuri ulioje ujira wa watendaji (wema). [Aal-'Imraan: 135-136]

وَتُوبُوا إِلَى اللَّـهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٣١﴾

Na tubuni kwa Allaah nyote, enyi Waumini mpate kufaulu. [An-Nuwr: 31]

 

وعن أبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم قال: (( مَنْ حَلَفَ فَقَالَ في حَلفِهِ : بِاللاَّتِ وَالعُزَّى ، فَلْيَقُلْ : لاَ إلَهَ إلاَّ اللهُ ، وَمَنْ قَالَ لِصَاحِبهِ : تَعَالَ أُقَامِركَ فَلْيَتَصَدَّقْ )) .متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Aliyekula kiapo na akasema katika kiapo chake kwa kutekeleza: 'Naapa kwa laata na 'uzzaa (hawa wawili walikuwa ni masanamu waliokuwa wakiabudiwa na Maquraysh wa Makkah kabla ya wao Kusilimu), basi aseme: 'Laa ilaaha illa Allaah (Hapana Mola Muabudiwa isipokuwa Allaah)'. Na mwenye kumwambia mwenzake, 'Njoo nicheze nawe kamari', basi atowe Swadaqah." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share