116-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuonywa katika Kufanya Aliyo Kataza Allaah 'Azza wa Jalla au Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب التحذير من ارتكاب
ما نهى الله عزوجل أَو رسوله صلى الله عليه وسلم عنه
116-Mlango Wa Kuonywa katika Kufanya Aliyo Kataza Allaah 'Azza wa Jalla au Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
قال الله تَعَالَى :
فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٦٣﴾
Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah au ikawasibu adhabu iumizayo. [An-Nuwr: 63]
وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ ۗ ﴿٣٠﴾
Na Allaah Anakutahadharisheni na Nafsi Yake [Aal-'Imraan: 30]
إِنَّ بَطْشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ ﴿١٢﴾
Hakika mkamato wa kuadhibu wa Rabb wako bila shaka ni mkali. [Al-Buruwj: 12]
وَكَذَٰلِكَ أَخْذُ رَبِّكَ إِذَا أَخَذَ الْقُرَىٰ وَهِيَ ظَالِمَةٌ ۚ إِنَّ أَخْذَهُ أَلِيمٌ شَدِيدٌ﴿١٠٢﴾
Na hivyo ndivyo Mkamato wa Rabb wako unavyokuwa Anapokamata miji na huku ikifanya dhulma. Hakika Mkamato Wake unaumiza vikali. [Huwd: 102]
وعن أبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم قالَ : (( إنَّ اللهَ تَعَالَى يَغَارُ ، وَغَيْرَة اللهِ ، أنْ يَأْتِيَ المَرْءُ مَا حَرَّمَ اللهُ عَلَيْهِ )) . متفق عليه .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Hakika Allaah Ta'aalaa, Hukasirika, na Hasira Zake zinachocheka (zinazidi kuwa kubwa) wakati mtu anapotenda yale yaliyokatazwa (yaliyoharamishwa) na Yeye Allaah." [Al-Bukhaariy]