114-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Mtu Kujinasibisha kwa Asiyekuwa Baba Yake na Mtumwa Anayemkimbia Bwana Wake
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تحريم انتساب الإنسان
إِلَى غير أَبيه وَتَولِّيه إِلَى غير مَواليه
114-Mlango Wa Uharamu wa Mtu Kujinasibisha kwa Asiyekuwa Baba Yake na Mtumwa Anayemkimbia Bwana Wake
Hadiyth – 1
عن سعد بن أَبي وقاص رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنِ ادَّعَى إِلَى غَيْرِ أبِيهِ وَهُوَ يَعْلَمُ أنَّهُ غَيْرُ أبِيهِ ، فالجَنَّةُ عَلَيْهِ حَرَامٌ )) . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Sa'ad bin Abu Waqqaas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kujinasibisha kwa asiyekuwa babake hali anaelewa kuwa hivyo si babake, basi itaharamishwa kwake Jannah." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لاَ تَرْغَبُوا عَنْ آبَائِكُمْ ، فَمَنْ رَغِبَ عَنْ أبِيهِ ، فَهُوَ كُفْرٌ )) . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msiwakatae baba zenu, atakayemkataa babake atakuwa amefanya tendo la ukafiri." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن يزيد بن شريكِ بن طارِقٍ ، قَالَ : رَأيتُ عَلِيّاً رضي الله عنه عَلَى المِنْبَرِ يَخْطُبُ ، فَسَمِعْتُهُ يقُولُ : لاَ واللهِ مَا عِنْدَنَا مِنْ كِتَابٍ نَقْرؤُهُ إِلاَّ كِتَابَ اللهِ ، وَمَا في هذِهِ الصَّحِيفَةِ ، فَنَشَرَهَا فَإذَا فِيهَا أَسْنَانُ الإبِلِ ، وَأشْيَاءُ مِنَ الجَرَاحَاتِ ، وَفِيهَا : قَالَ رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( المَدينَةُ حَرَمٌ مَا بَيْنَ عَيْرٍ إِلَى ثَوْرٍ ، فَمَنْ أحْدَثَ فِيهَا حَدَثاً ، أَوْ آوَى مُحْدِثاً ، فَعَلَيْهِ لَعْنَةُ اللهِ وَالمَلاَئِكَةِ وَالنَّاسِ أجْمَعِينَ ، لاَ يَقْبَلُ اللهُ مِنْهُ يَومَ القِيَامَةِ صَرْفاً وَلاَ عَدْلاً . ذِمَّةُ المُسْلِمينَ وَاحِدَةٌ ، يَسْعَى بِهَا أَدْنَاهُمْ ، فَمَنْ أَخْفَرَ مُسْلِماً ، فَعَلَيْهِ لَعْنَةُ اللهِ وَالمَلائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ، لاَ يَقْبَلُ اللهُ مِنْهُ يَومَ القِيَامَةِ صَرْفاً وَلاَ عَدْلاً . وَمَن ادَّعَى إِلَى غَيرِ أَبيهِ ، أَوْ انْتَمَى إِلَى غَيرِ مَوَاليهِ ، فَعَلَيْهِ لَعْنَةُ اللهِ وَالمَلاَئِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعينَ ؛ لاَ يَقْبَلُ اللهُ مِنْهُ يَومَ القِيَامَةِ صَرْفاً وَلاَ عَدْلاً )) . متفق عَلَيْهِ .
Amesema Yaziyd bin Shariyk bin Twaariq: Nilimuona 'Ali (Radhwiya Allaahu 'anhu) juu ya minbar akihutubu, nikamsikia akisema: "Naapa kwa Allaah! Hatuna kitabu chengine tunacho kisoma isipokuwa Kitabu cha Allaah (Qur-aan) na zilizomo ndani ya sahifa. Tunapofungua Kitabu hichi tunapata maelezo ya miaka ya ngamia (viwango vya zakah) na mambo yanayohusu fidia ya jeraha (damu iliyo mwagwa). Na pia kinataja kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: 'Madiynah ni mji mtukufu baina ya majabali mawili ya 'Ayr na Thawr. Mwenye kuzua ndani yake au akampatia makao (himaya) mzushi, atakuwa na laana ya Allaah na Malaaikah na watu wote. Allaah Hatakubali kutoka kwake Siku ya Qiyaamah toba yake wala fidia. Dhamana ya Waislamu wote ni moja (kwani hadhi na majukumu yao yako sawa) wala chini kabisa miongoni mwao anaweza kutoa himaya. Yeyote mwenye kuvunja himaya aliyopewa na kumtweza Muislamu, juu yake laana ya Allaah, na Malaaikah na watu wote. Allaah Hatakubali kutoka kwake Siku ya Qiyaamah toba yake wala fidia. Na mwenye kujinasibisha kwa asiyekuwa baba yake au mtumwa anayekimbia na kwenda kwa bwana mwengine, ni juu yake laana ya Allaah, na Malaaikah na wtau wote. Allaah Hatakubali kutoka kwake Siku ya Qiyaamah toba yake wala fidia." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن أَبي ذَرٍّ رضي الله عنه : أنَّه سَمِعَ رَسُولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( لَيْسَ مِنْ رَجُلٍ ادَّعَى لِغَيرِ أَبِيهِ وَهُوَ يَعْلَمُهُ إِلاَّ كَفَرَ ، وَمَنِ ادَّعَى مَا لَيْسَ لَهُ ، فَلَيْسَ مِنَّا ، وَلَيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنَ النَّارِ ، وَمَنْ دَعَا رَجُلاً بالكُفْرِ ، أَوْ قَالَ : عَدُو اللهِ ، وَلَيْسَ كَذَلِكَ إِلاَّ حَارَ عَلَيْهِ )) . متفق عَلَيْهِ ، وهذا لفظ رواية مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Haitokei kwa mtu kujinasibisha na asiyekuwa baba yake hali anamuelewa isipokuwa amekufuru. Na mwenye kujinasibisha kwa kitu kisichokuwa chake, si katika sisi, basi ajiandalie makazi yake motoni. Na menye kumnasibisha mtu na ukafiri au akamwambia: 'Adui wa Allaah', naye si hivyo isipokuwa ukafiri hurudi kwake." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hili ni tamshi la Muslim]