113-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kukaa Kimya Kuanzia Asubuhi Mpaka Usiku
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن صمت يوم إلَى الليل
113-Mlango Wa Kukatazwa Kukaa Kimya Kuanzia Asubuhi Mpaka Usiku
Hadiyth – 1
عن عليٍّ رضي الله عنه قَالَ : حَفِظْتُ عَنْ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( لاَ يُتْمَ بَعْدَ احْتِلاَمٍ ، وَلاَ صُمَاتَ يَومٍ إِلَى اللَّيْلِ )) . رواه أَبُو داود بإسناد حسن .
Kutoka kwa 'Ali (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nimehifadhi kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hakuna anayebaki kuwa yatima baada kubaleghe wala hakuna maana kunyamaza (kuwa kimya bila kuzungumza) kuanzia asubuhi mpaka usiku." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Hasan]. Amesema Al-Khattwaabiy katika kuitafsiri hii Hadiyth: "Ilikuwa miongoni mwa sifa za Kijahiliya kunyamaza, Uislamu ukakataza jambo hilo na kuwaamuru watu wawe ni wenye kumdhukuru Allaah na kuzungumza mazungumzo ya kheri."
Hadiyth – 2
وعن قيس بن أَبي حازم ، قَالَ : دَخَلَ أَبُو بكر الصِّدِّيق رضي الله عنه عَلَى امْرأَةٍ مِنْ أحْمَسَ يُقَالُ لَهَا : زَيْنَبُ ، فَرَآهَا لاَ تَتَكَلَّمُ . فَقَالَ : مَا لَهَا لا تتكلمُ ؟ فقالوا : حَجَّتْ مصمِتةً ، فقالَ لها : تَكَلَّمِي ، فَإنَّ هَذَا لاَ يَحِلُّ ، هَذَا مِنْ عَمَلِ الجَاهِليَّةِ ، فَتَكَلَّمَتْ . رواه البخاري .
Amesema Qays bin Abu Haazim: Aliingia Abu Bakar Asw-Swiddiq (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa mwanamke mmoja wa kabila la Ahmas aliyekuwa akiitwa Zaynab na kumuona hazungumzi. Akauliza: "Ana nini mbona hazungumzi?" Wakamjibu: "Ameapa kukaa kimya." Akamwambia: "Zungumza kwani jambo hilo si halali na ni amali za siku za Ujahiliya." Hapo akaanza kuzungumza. [Al-Bukhaariy]