112-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Mwanamume Kuvaa Nguo ya Zafarani

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب تحريم لبس الرجل ثوباً مزعفراً

112-Mlango Wa Uharamu wa Mwanamume Kuvaa Nguo ya Zafarani

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن أنس رضي الله عنه قَالَ : نَهَى النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنْ يَتَزَعْفَرَ الرجُل . متفق عَلَيْهِ .

Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza mwanamume kutumia zafarani. [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuwd]

 

Hadiyth – 2

وعن عبد اللهِ بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : رأى النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَيَّ ثَوْبَيْنِ مُعَصْفَرَيْنِ ، فَقَالَ : (( أُمُّكَ أمَرَتْكَ بِهَذا ؟ )) قلتُ: أَغْسِلُهُمَا ؟ قَالَ: (( بَلْ أَحْرِقْهُمَا )) .

وفي رواية ، فَقَالَ : (( إنَّ هَذَا مِنْ ثِيَابِ الكُفَّارِ فَلاَ تَلْبَسْهَا )) . رواه مسلم .

Amesema 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniona nikiwa nimevaa vipande viwili vya nguo ya zafarani (rangi ya manjano). Akaniuliza: "Je, mamako ndiye aliyekuamuru kuvaa hizi?" Nikasema: "Je, nizifue?" Akasema: "Zichome." 

Na katika riwaayah nyengine, alisema: "Hakika hizi ni katika nguo za makafiri, hivyo usuzivae." [Muslim]

 

 

 

 

Share