111-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Kutumia Vyombo vya Dhahabu, Fedha katika Kula, Kunywa, Tohara na Njia Zote za Matumizi yake
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تحريم استعمال إناء الذهب وإناء الفضة
في الأكل والشرب والطهارة وسائر وجوه الاستعمال
111-Mlango Wa Uharamu wa Kutumia Vyombo vya Dhahabu, Fedha katika Kula, Kunywa, Tohara na Njia Zote za Matumizi yake
Hadiyth – 1
عن أُمِّ سلمة رَضِيَ اللهُ عنها : أنَّ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( الَّذِي يَشْرَبُ في آنِيَةِ الفِضَّةِ ، إنَّمَا يُجَرْجِرُ في بَطْنِهِ نَارَ جَهَنَّمَ )) متفق عَلَيْهِ .
وفي رواية لمسلم : (( إنَّ الَّذِي يَأكُلُ أَوْ يَشْرَبُ في آنِيَةِ الفِضَّةِ والذَّهَبِ )) .
Imepokewa kutoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anayekunywa katika chombo cha fedha anaangushia moto tumboni mwake." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]
Na katika riwaayah ya Muslim: "Hakika anayekula au kunywa katika chombo cha fedha na dhahabu."
Hadiyth – 2
وعن حُذَيفَةَ رَضِيَ اللهُ عنه ، قَالَ : إنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم نهانا عنِ الحَريِرِ ، وَالدِّيبَاجِ ، وَالشُّرْبِ في آنِيَةِ الذَّهَبِ وَالفِضَّةِ ، وقالَ : (( هُنَّ لَهُمْ في الدُّنْيَا ، وَهِيَ لَكُمْ فِي الآخِرَةِ )) . متفق عَلَيْهِ .
وفي رواية في الصحيحين عن حُذيْفَةَ رَضِيَ اللهُ عنه : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( لاَ تَلْبسُوا الحَرِيرَ وَلاَ الدِّيبَاجَ ، وَلاَ تَشْرَبُوا فِي آنِيَةِ الذَّهَبِ وَالفِضَّةِ وَلاَ تَأكُلُوا في صِحَافِهَا )) .
Amesema Hudhayfah (Radhyewiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametukataza kuvaa hariri na dibaji na kunywa katika vyombo vya dhahabu na fedha na akasema: "Vitu hivyo ni vyao hapa duniani na ni vyenu Aakherah." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na katika riwaayah nyengine katika Swahiyh mbili kutoka kwa Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Musivae nguo za hariri wala dibaji wala musinywe katika vyombo vya dhahabu na fedha wala musile katika sinia zake."
Hadiyth – 3
وعن أنس بن سِيِرين ، قَالَ : كنتُ مَعَ أنس بن مالك رَضِيَ اللهُ عنه ، عِنْدَ نَفَرٍ مِنَ المَجُوسِ ؛ فَجِيءَ بفَالُوذَجٍ عَلَى إنَاءٍ مِنْ فِضَّةٍ ، فَلَمْ يَأَكُلْهُ ، فَقِيلَ لَهُ : حَوِّلْهُ ، فَحَوَّلَهُ عَلَى إناءٍ مِنْ خَلَنْجٍ وَجِيءَ بِهِ فَأَكَلَهُ . رواه البيهقي بإسناد حسن .
Amesema Anas bin Siyriyn: Nilikuwa na Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) pamoja na baadhi ya Majusai. Mara ikaletwa tamutamu katika chombo cha fedha, naye (Radhwiya Allaahu 'anhu) akakataa kula ndani yake. Yule aliyeleta aliambiwa abadilishe chombo hicho, naye akafanya hivyo na kuleta (tamutamu hiyo) katika chombo cha Khalanj (ni mti ulio na rangi baina ya majano na nyekundu ambao mbao zake hutumiwa kutengeneza vyombo) na Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) akala. [Al-Bayhaqiy kwa Isnaad iliyo Hasan]