008-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume:Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Ni Haramu Kuvaa Nguo Ya Kipekee Ili Kuonekana Tofauti (Vazi La Umashuhuri)
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
008- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Ni Haramu Kuvaa Nguo Ya Kipekee Ili Kuonekana Tofauti (Vazi La Umashuhuri):
Ibn ‘Umar amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَنْ لَبِسَ ثَوْبَ شُهْرَةٍ فيٍ الدُّنْيَا أَلْبَسَهُ اللَّهُ ثَوْبَ مَذَلَّةٍ يَوْمَ الْقِيَامَةِ" [ثُمَّ أَلْهَبَ فِيْهِ نَارًا]
“Mwenye kuvaa nguo ya kutaka yeye pekee aonekane tofauti na wengine hapa duniani, Allaah Atamvisha nguo ya udhalili Siku ya Qiyaamah [Kisha Atamwashia ndani yake moto]. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4029), Ibn Maajah (3606) na Ahmad (2/92), iko kwenye Swahiyhul Jaami’i (6526)].
Ibn Al-Athiyr amesema: “Nguo hii, ni nguo ya mtu kutaka umashuhuri kati ya watu, rangi yake iwe tofauti na rangi ya nguo zao (au mshono, kitambaa n.k) kiasi cha kuwafanya watu wanyanyue macho yao kuiangalia huku akitamba kwa kiburi na kujiona yeye ni yeye, hakuna zaidi yake”.