03-Malaika: Jogoo Ana Uwezo Wa Kumwona Malaika

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

 

 

03:  Jogoo Ana Uwezo Wa Kumuona Malaika

 

 

 

Kati ya yenye kuthibitisha uwepo wa Malaika, ni Hadiyth ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) iliyosimuliwa na Abu Hurayrah isemayo:

 

"إِذَا سَمِعْتُمْ صِيَاحَ الدِّيَكَةِ فَاسْأَلُوا اللَّهَ مِنْ فَضْلِهِ؛ فَإِنَّهَا رَأَتْ مَلَكاً وَإِذَا سَمِعْتُمْ نَهِيقَ الْحِمَارِ فَتَعَوَّذُوا بِاللَّهِ مِنَ الشَّيطَانِ؛ فَإِنَّهُ رَأَى شَيْطَاناً"

 

“Mnaposikia jogoo wanawika, basi muombeni Allaah Fadhla Zake, kwani kwa hakika wamemwona Malaika.  Na mnaposikia sauti kali ya punda, basi jilindeni kwa Allaah kutokana na shaytwaan, kwani kwa hakika amemwona shaytwaan”.  [Al-Bukhaariy (3303) na Muslim (2729)]

 

Hizo ni sifa ambazo kwazo jogoo na punda wamemzidi mwanadamu wa kuwa na uwezo wa kuona ambavyo mwanadamu hawezi kuviona.  Hivyo basi, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) anatuelekeza kwamba tukimsikia jogoo anawika, basi hapo hapo tumwombe Allaah Fadhla Zake, kwani jogoo kamuona Malaika.  Tuseme kwa mfano:

 

"اللَّهمَّ إنَّا نَسأَلُك مِن فَضلِك"

 

“Ee Allaah!  Hakika sisi tunakuomba Fadhla Zako”.

 

Kwa kuwa hapo kuna matumaini makubwa ya Malaika huyo kuitikia “Aamiyn” kwa duaa hiyo na kumwombea mtu maghfira, lakini pia kumshuhudilia ikhlaasi yake kwa Allaah.  Na hapo duaa zinavaana pamoja na Allaah Anajibu.

 

Vile vile, tunaposikia punda analia kwa sauti yake kali ya kubughudhi, basi hapo tujilinde kwa Allaah na shaytwaan aliyewekwa mbali na Rahmah za Allaah, kwa kuwa shaytwaan anakuwa yuko eneo hilo.  Hivyo tunatakiwa tujilinde kutokana na shari zake na ushawishi wake.

 

 

 

Share