07-Malaika: Malaika Miykaaiyl

 

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

07:  Malaika Miykaaiyl

 

Allaah Ta’aalaa Amesema:

 

 "مَنْ كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ"

 

“Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake, na Rusuli Wake, na Jibriyl, na Miykaala, basi hakika Allaah Ni adui kwa makafiri”.   [Al-Baqarah: 98].

 

Miykaaiyl ametajwa katika aayaah hii pamoja na Jibriyl (‘Alayhis salaam) kwa kuwa Mayahudi walidai kwamba Jibriyl ni adui yao, lakini Miykaaiyl ni kipenzi chao.  Na hapa Allaah Anawajulisha kuwa yeyote kati yao atakayemfanya Jibriyl ni adui, basi amewafanya Malaika wote kuwa maadui.  Lakini pia amemfanya Allaah kuwa adui.  Na hili ni jambo la hatari kabisa.  Muislamu anatakiwa atahadhari sana na itikadi kama hizi.

 

Malaika Miykaaiyl ndiye anayesimamia suala la mvua na riziki kwa viumbe.  Na mbali na kutajwa kwenye aayah hii, pia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam amemtaja katika duaa yake katika Hadiyth iliyoelezewa na Bibi ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa):

 

"كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَامَ مِنَ اللَّيْلِ افْتَتَحَ صَلَاتَهُ فَقَالَ: اللَّهُمَّ رَبَّ جِبْرِيلَ وَمِيكَائِيلَ وَإِسْرَافِيلَ ، فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ، عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ"

 

“Alikuwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anaposimama usiku, anaifungua swalah yake kwa kusema:  “Ee Allaah! Mola wa Jibriyl, Miykaaiyl, na Israafiyl, Muumba wa mbingu na ardhi, Unayejua yaliyofichikana na yenye kuonekana..”  [Muslim (628). Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh].

 

 

Share