26-Malaika: Makazi Ya Malaika

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

 

26:  Makazi Ya Malaika

 

Makazi na mashukio ya Malaika ni mbinguni.  Bibi ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) alimsikia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:

 

"إنَّ المَلَائِكَةَ تَنْزِلُ في العَنَانِ: وهو السَّحَابُ، فَتَذْكُرُ الأمْرَ قُضِيَ في السَّمَاءِ، فَتَسْتَرِقُ الشَّيَاطِينُ السَّمْعَ فَتَسْمَعُهُ، فَتُوحِيهِ إلى الكُهَّانِ، فَيَكْذِبُونَ معهَا مِئَةَ كَذْبَةٍ مِن عِندِ أنْفُسِهِمْ"

 

“Hakika Malaika hushuka kwenye anga za karibu wakaelezana jambo lililopitishwa mbinguni.  Mashetani hudukua wakapata kusikiliza wanayoyasema, halafu huja kuwapasha habari makuhani na kuongeza kwenye habari moja uongo 100 kutoka kwao”.  [Al-Bukhaariy: (3210)]

 

Abu Hurayrah:  “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"إذا قالَ أحَدُكُمْ: آمِينَ، وقالتِ المَلائِكَةُ في السَّماءِ: آمِينَ، فَوافَقَتْ إحْداهُما الأُخْرَى غُفِرَ له ما تَقَدَّمَ مِن ذَنْبِهِ"

 

“Akisema mmoja wenu aamiyn, na Malaika mbinguni wakasema aamiyn, na aamiyn zote mbili zikakutana, basi husamehewa dhambi zake zilizotangulia”.  [Hadiyth Swahiyh:  Al-Bukhaariy (781) na Muslim (410)]

 

Ibn Kathiyr amesema:  “Hakuna mahala popote katika mbingu saba isipokuwa wako Malaika.  Kati yao wako walio simama daima, wako walio rukuu daima, na wako wenye kusujudu daima, na wako wengine wa aina nyingine ambao Allaah Pekee Ndiye Anaowajua”.

 

As-Suyuwtwiy amesema:  “Mbingu ndio makazi yao na mahala pao kama yalivyo mabustani mazuri kwa upande wa ardhi”.

 

 

Share