29-Malaika: Malaika Ni Waja Wa Allaah Na Hawana Sifa Za Kiola

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

29:  Malaika Ni Waja Wa Allaah Na Hawana Sifa Za Kiola

 

Malaika ni waja wa Allaah na hawana sifa zozote za kimola au kiungu, nao wanamwogopa Allaah ukweli wa kumwogopa.  Allaah Ta’alaa Anasema:

 

"مَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُؤْتِيَهُ اللَّـهُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُوا عِبَادًا لِّي مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِن كُونُوا رَبَّانِيِّينَ بِمَا كُنتُمْ تُعَلِّمُونَ الْكِتَابَ وَبِمَا كُنتُمْ تَدْرُسُونَ وَلَا يَأْمُرَكُمْ أَن تَتَّخِذُوا الْمَلَائِكَةَ وَالنَّبِيِّينَ أَرْبَابًا ۗ أَيَأْمُرُكُم بِالْكُفْرِ بَعْدَ إِذْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ"

 

“Ni mustahili kwa mtu kwamba Allaah Amempa Kitabu na Al-Hukma na Unabii kisha aje awaambie watu:  Kuweni wenye kuniabudu mimi badala ya Allaah, bali (atawaambia): Kuweni Wanachuoni waswalihina kwa yale mliyokuwa mkiyafundisha ya Kitabu na kwa yale mliyokuwa mkiyadurusu.  ● Na wala hakuamuruni kuwachukua Malaika na Manabii kuwafanya miola. Je, anakuamrisheni ukafiri baada ya nyinyi kuwa mmejisalimisha kwa Allaah?”   [Aal ‘Imraan: 79-80]

 

Hapa Allaah Ta’aalaa Anabainisha kwamba kuwafanya Malaika na Mitume waola ni kufru.  Na yeyote atakayewafanya Malaika au Mitume hivyo, akawaomba wamletee manufaa au wamwondoshee madhara, au wamsamehe dhambi zake, au waongoe moyo wake au wamsaidie kumletea faraja kwa misukosuko inayomkabili, basi mtu huyo ni kafiri kwa itifaki ya Waislamu.

 

Allaah Ta’alaa Anasema:

 

"وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَـٰنُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۚ بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ لَا يَسْبِقُونَهُ بِالْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِ يَعْمَلُونَ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ وَهُم مِّنْ خَشْيَتِهِ مُشْفِقُونَ وَمَن يَقُلْ مِنْهُمْ إِنِّي إِلَـٰهٌ مِّن دُونِهِ فَذَٰلِكَ نَجْزِيهِ جَهَنَّمَ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ"

 

Na wakasema:  Ar-Rahmaan Amejifanyia mwana!  Subhaanah!  Utakasifu ni Wake!  Bali (hao) ni waja waliokirimiwa ●  Hawamtangulii (Allaah) kwa kauli, nao kwa Amri Yake wanatenda ●  Anajua yale yaliyoko mbele yao, na yale yaliyoko nyuma yao, na wala hawataomba shafaa’ah (yeyote) isipokuwa kwa yule ambaye (Allaah) Amemridhia, nao kutokana na kumkhofu, ni wenye khofu na kutahadhari  ● Na yeyote yule miongoni mwao atakayesema:  Mimi ni mwabudiwa badala Yake, basi huyo Tutamlipa Jahannam.  Hivyo ndivyo Tunavyolipa madhalimu”.   [Al-Anbiyaa: 26-29]

 

As- Sa’adiy amesema:  “Allaah Ta’aalaa Anatueleza katika Aayaat hizi kuhusu sifa za Malaika.  Anatuambia kwamba Malaika ni waja waliokirimiwa, na wao wanaendeshwa kama walivyo viumbe wote.  Lakini pia ni viumbe waliotakaswa kutokana na machafu, wamefikia ukomo wa mwisho wa kumheshimu Allaah, nao wanatekeleza Maamrisho Yake yote.  Hawasemi jambo lolote bila ya amri toka kwa Allaah na hawawezi kufanya lolote kwa utashi wao bila maelekezo toka kwa Allaah Ta’alaa”.

 

Hivyo basi, Malaika hawa ni sehemu ya viumbe wa Allaah walio chini ya mamlaka Yake.  Hawana uwezo wa kufanya lolote ila lile tu walilowezeshwa na Allaah Ta’aalaa.

 

Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) amesema:  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Jibriyl:

 

"أَلاَ تَزُورُنَا أَكْثَرَ مِمَّا تَزُورُنَا؟ ‏‏ قَالَ: فَنَزَلَتْ: ‏‏وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلاَّ بِأَمْرِ رَبِّكَ لَهُ مَا بَيْنَ أَيْدِينَا وَمَا خَلْفَنَا‏"‏ 

 

“Mbona hututembelei zaidi ya unavyotutembelea?  Hapo ikashuka Kauli Yake Taalaa:

 

 “Na (sisi Malaika) hatuteremki ila kwa Amri ya Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).  Ni Yake Yeye yaliyoko mbele yetu, na yaliyoko nyuma yetu".  [Al-Bukhaariy (3218) na Muslim (3158)]

 

 

Share