46-Malaika: Kazi Za Malaika: (9)- Malaika Wanaozunguka Kwenye Njia Na Barabara Kutafuta Majaalis Za Dhikr

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

46:   Kazi Za Malaika  

 

(9)- Malaika Wanaozunguka Kwenye Njia Na Barabara Kutafuta Majaalis Za Dhikr

 

Malaika hawa hawana kazi nyingine isipokuwa kuzunguka huku na kule kuwatafuta watu waliokaa pamoja kwa ajili ya kumdhukuru Allaah.  Wakiwapata, huwazunguka kwa mbawa zao, huwaombea maghfira na husikiliza adhkaar zao.

Abu Hurayrah amesema:  “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"إِنَّ لِلَّهِ مَلاَئِكَةً يَطُوفُونَ فِي الطُّرُقِ، يَلْتَمِسُونَ أَهْلَ الذِّكْرِ، فَإِذَا وَجَدُوا قَوْمًا يَذْكُرُونَ اللَّهَ تَنَادَوْا هَلُمُّوا إِلَى حَاجَتِكُمْ‏.‏ قَالَ: فَيَحُفُّونَهُمْ بِأَجْنِحَتِهِمْ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا‏.‏ قَالَ: فَيَسْأَلُهُمْ رَبُّهُمْ وَهُوَ أَعْلَمُ مِنْهُمْ: مَا يَقُولُ عِبَادِي؟ قَالُوا: يَقُولُونَ يُسَبِّحُونَكَ، وَيُكَبِّرُونَكَ، وَيَحْمَدُونَكَ وَيُمَجِّدُونَكَ‏.‏ قَالَ: فَيَقُولُ هَلْ رَأَوْنِي؟ قَالَ: فَيَقُولُونَ لاَ وَاللَّهِ مَا رَأَوْكَ‏.‏ قَالَ: فَيَقُولُ وَكَيْفَ لَوْ رَأَوْنِي؟ قَالَ: يَقُولُونَ لَوْ رَأَوْكَ كَانُوا أَشَدَّ لَكَ عِبَادَةً، وَأَشَدَّ لَكَ تَمْجِيدًا، وَأَكْثَرَ لَكَ تَسْبِيحًا‏.‏ قَالَ: يَقُولُ فَمَا يَسْأَلُونِي قَالَ يَسْأَلُونَكَ الْجَنَّةَ‏.‏ قَالَ: يَقُولُ وَهَلْ رَأَوْهَا؟ قَالَ: يَقُولُونَ لاَ وَاللَّهِ يَا رَبِّ مَا رَأَوْهَا‏.‏ قَالَ: يَقُولُ فَكَيْفَ لَوْ أَنَّهُمْ رَأَوْهَا؟ قَالَ: يَقُولُونَ لَوْ أَنَّهُمْ رَأَوْهَا كَانُوا أَشَدَّ عَلَيْهَا حِرْصًا، وَأَشَدَّ لَهَا طَلَبًا، وَأَعْظَمَ فِيهَا رَغْبَةً‏.‏ قَالَ: فَمِمَّ يَتَعَوَّذُونَ؟ قَالَ: يَقُولُونَ مِنَ النَّارِ‏.‏ قَالَ: يَقُولُ وَهَلْ رَأَوْهَا؟ قَالَ: يَقُولُونَ لاَ وَاللَّهِ مَا رَأَوْهَا‏.‏ قَالَ: يَقُولُ فَكَيْفَ لَوْ رَأَوْهَا؟ قَالَ: يَقُولُونَ لَوْ رَأَوْهَا كَانُوا أَشَدَّ مِنْهَا فِرَارًا، وَأَشَدَّ لَهَا مَخَافَةً‏.‏ قَالَ: فَيَقُولُ فَأُشْهِدُكُمْ أَنِّي قَدْ غَفَرْتُ لَهُمْ‏.‏ قَالَ: يَقُولُ مَلَكٌ مِنَ الْمَلاَئِكَةِ فِيهِمْ فُلاَنٌ لَيْسَ مِنْهُمْ إِنَّمَا جَاءَ لِحَاجَةٍ‏.‏ قَالَ: هُمُ الْجُلَسَاءُ لاَ يَشْقَى بِهِمْ جَلِيسُهُمْ ‏"‏‏.‏ 

 

“Hakika Allaah Ana Malaika wanaozunguka majiani kuwatafuta watu wa dhikri.  Wanapowapata watu wanaomdhukuru Allaah huitana wakisema:  Haya njooni kwenye lile mlitafutalo.  Na hapo huwazungushia mbawa zao hadi kwenye mbingu ya dunia.  Halafu Mola wao Huwauliza nailhali Yeye Anajua zaidi kuliko wao:  Waja Wangu wanasema nini?  Malaika hujibu wakisema:  Wanakutakasa, wanakukabirisha, wanakuhimidi na wanakutukuza.  Allaah Huwauliza:  Je, wameniona?  Malaika hujibu:  Hapana, tunaapa kwa Jina Lako.  Allaah Huwaambia:  Ingekuwaje kama wangeniona?  Hujibu:  Kama wangelikuona, basi wangelikuabudu kwa nguvu zaidi, wangelikutukuza na kukuhimidi zaidi, na wangelikutakasa kwa wingi zaidi.  Allaah Huwauliza tena:  Wananiomba nini?  Husema:  Wanakuomba Jannah.  Huwauliza:  Je, wameiona?  Wanajibu:  Hapana wa-Allaah, ee Mola wetu, hawajaiona.  Huwaambia:  Itakuwa vipi lau wangelioona?  Hujibu:  Kama wangeliiona, basi wangelikuwa na pupa nayo zaidi, wangekuwa na haja nayo zaidi, na utashi mkubwa nayo zaidi.  Huwauliza:  Ni kitu gani wanajilinda nacho?  Hujibu:  Wanajilinda na moto.  Huwauliza:  Je, wameuona?  Hujibu:   Hapana wa-Allaah, ee Mola wetu, hawajauona.   Huwauliza:  Ingekuwa vipi lau wangeliuona?  Hujibu:  Wangeliuona, basi wangeliukimbia kwa nguvu zao zote na wangeliuogopa zaidi.  Huwaambia:  Basi Nakushuhudilieni kwamba Mimi Nimewasamehe.  Malaika mmoja atasema:  Yuko fulani, si katika wao, yeye amekuja tu kwa haja nyingine.  Allaah Atamwambia: Wote hao ni wa majilisi moja, anayekaa nao hataadhibiwa”.  [Swahiyhul Bukhaariy (6408)]   

 

Abu Hurayrah amesema tena:  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: 

 

"مَا اجْتَمَعَ قَوْمٌ فِي بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللَّهِ تَعَالَى يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَيَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ إِلاَّ نَزَلَتْ عَلَيْهِمُ السَّكِينَةُ وَغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ وَحَفَّتْهُمُ الْمَلاَئِكَةُ وَذَكَرَهُمُ اللَّهُ فِيمَنْ عِنْدَهُ ‏"‏ ‏.‏

 

“Hawakusanyiki watu katika Nyumba yoyote katika Nyumba za Allaah ili kusoma na kufundishana Kitabu cha Allaah, isipokuwa huwateremkia utulivu,  rahmah huwafunika, Malaika huwazunguka, na Allaah Huwataja kwa wale walio Kwake”.  [Muslim (2699)]

  

Ibn ‘Uthaymiyn amesema:  “Miongoni mwa faida za Hadiyth hii ni kwamba Allaah Anawatumikisha Malaika Wake kwa ajili ya mwanadamu, na hapa Waumini hawa wanaosoma Kitabu cha Allaah, wanapata utukuzo na hishma kubwa ya kuzungukwa na Malaika hao”.

 

Bila shaka hali kama hii haimruhusu shaytwaan kukurubia. 

 

 

Share