50-Malaika: Kazi Za Malaika: (13)- Malaika Wasimamizi Na Walinzi Wa Pepo

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

50:   Kazi Za Malaika  

 

(13)- Malaika Wasimamizi Na Walinzi Wa Pepo

                                                        

Allaah Ta’aalaa Amesema:

 

"وَسِيقَ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ إِلَى الْجَنَّةِ زُمَرًا ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوهَا وَفُتِحَتْ أَبْوَابُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا سَلَامٌ عَلَيْكُمْ طِبْتُمْ فَادْخُلُوهَا خَالِدِينَ"

 

Na wataongozwa wale waliomcha Rabb wao kuelekea Jannah makundi-makundi, mpaka watakapoifikia na milango yake ishafunguliwa, na walinzi wake watawaambia:  Salaamun ‘Alaykum!  Amani iwe juu yenu, furahini na iingieni, mdumu milele.  [Az-Zumar: 73]

 

Aayaah hii na aayah ya 71 ya Suwrah hii, ni dalili kwamba Pepo na Moto zina milango inayofungwa na kufunguliwa, na kila moja ina walinzi na wasimamizi wake.

 

Katika Hadiyth ya Anas, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"آتي بابَ الجَنَّةِ يَومَ القِيامَةِ فأسْتفْتِحُ، فيَقولُ الخازِنُ: مَن أنْتَ؟ فأقُولُ: مُحَمَّدٌ، فيَقولُ: بكَ أُمِرْتُ لا أفْتَحُ لأحَدٍ قَبْلَكَ"  

 

“Nitauendea mlango wa Pepo Siku ya Qiyaamah na kubisha.  Mlinzi wake atauliza:  Nani wewe?  Nitamjibu:  Muhammad.  Atasema:  Ni wewe tu nimeamrishwa kufungua, simfungulii yeyote kabla yako”.  [Swahiyh Muslim: 197]

 

Hadiyth hii ni dalili pia kwamba Malaika wako makini sana katika kazi na majukumu yao.

 

 

Share