66-Malaika: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini: (14)– Malaika Wanamlinda Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Dhidi Ya Maadui Zake

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

66:   Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini  

 

(14)– Malaika Wanamlinda Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Dhidi Ya Maadui Zake

 

Malaika hubeba jukumu la kumlinda Rasuli wa Allaah na Rusuli wengineo kutokana na njama za maadui na makafiri. Abu Hurayrah amesema: 

 

"قَالَ أَبُو جَهْلٍ: هَلْ يُعَفِّرُ مُحَمَّدٌ وَجْهَهُ بَيْنَ أَظْهُرِكُمْ؟ قَالَ: فَقِيلَ نَعَمْ ‏.‏ فَقَالَ: وَاللاَّتِ وَالْعُزَّى لَئِنْ رَأَيْتُهُ يَفْعَلُ ذَلِكَ لأَطَأَنَّ عَلَى رَقَبَتِهِ أَوْ لأُعَفِّرَنَّ وَجْهَهُ فِي التُّرَابِ،  قَالَ: فَأَتَى رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يُصَلِّي زَعَمَ لِيَطَأَ عَلَى رَقَبَتِهِ، قَالَ: فَمَا فَجِئَهُمْ مِنْهُ إِلاَّ وَهُوَ يَنْكِصُ عَلَى عَقِبَيْهِ وَيَتَّقِي بِيَدَيْهِ - قَالَ - فَقِيلَ لَهُ مَا لَكَ فَقَالَ إِنَّ بَيْنِي وَبَيْنَهُ لَخَنْدَقًا مِنْ نَارٍ وَهَوْلاً وَأَجْنِحَةً ‏.‏ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ لَوْ دَنَا مِنِّي لاَخْتَطَفَتْهُ الْمَلاَئِكَةُ عُضْوًا عُضْوًا ‏"‏ ‏.

 

“Abu Jahl aliuliza wenzake:  Je, (mnamwona) Muhammad akiuweka uso wake mchangani na nyinyi mnamtazama?  Akaambiwa na’am.  Akasema:  Naapa kwa Al-Laati na Al-‘Uzzaa, lau nitamwona anafanya hivyo, basi nitaikanyaga shingo yake na kuigaragazisha mchangani. Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa anaswali, alimwendea ili aikanyage shingo yake (atakaposujudu). Hapo wenzake walishtukizwa kumwona anarudi kinyume nyume (kwa hofu) huku anazuilia (kitu) kwa mikono yake.  Wakamuuliza:  Una nini?  Mbona hivyo?  Akasema:  Hakika kuna shimo refu la moto kati yangu mimi na yeye, na kuna kitu cha kutisha pamoja na mbawa.  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:  Lau angenikurubia, basi Malaika wangemnyofoa kiungo kimoja kimoja”.   [Swahiyh Muslim: (2797)] 

 

 

Share