67-Malaika: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini: (15)– Wanahudhuria Mazishi Ya Baadhi Ya Watu Wema

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

67:   Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini  

 

(15)– Wanahudhuria Mazishi Ya Baadhi Ya Watu Wema

 

Alipokufa Swahaba mtukufu Sa’ad bin Mu’aadh, Malaika wapatao elfu sabini walishuhudia mazishi yake.  Toka kwa Ibn ‘Umar:  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema kuhusu Sa’ad bin Mu’aadh (Radhwiya Allaah ‘anhu) wakati alipokufa:

 

"هَذَا الَّذِي تَحَرَّكَ لَهُ الْعَرْشُ وَفُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَشَهِدَهُ سَبْعُونَ أَلْفًا مِنْ الْمَلَائِكَةِ ، لَقَدْ ضُمَّ ضَمَّةً ثُمَّ فُرِّجَ عَنْهُ"

 

“Huyu ndiye ambaye ‘Arshi ilitikisika kwa ajili yake, milango ya mbingu ikafunguliwa kwa ajili yake, na  Malaika elfu 70 walishuhudia mazishi yake, huyu (aliyefanyiwa yote haya) amebanwa akabanika, kisha akaachiliwa”.   [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh katika “Swahiyh An-Nasaaiy”].

 

 

 

Share