70-Malaika: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini: (18)– Malaika Watailinda Makkah Na Madiynah Kutokana Na Dajjaal

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

70:   Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini

 

(18)– Malaika Watailinda Makkah Na Madiynah Kutokana Na Dajjaal

 

Al-Masiyh Ad Dajjaal atakapodhihiri, ataingia miji yote isipokuwa Makkah na Madiynah kwa kuwa itakuwa inalindwa na Malaika. 

 

Katika kisa cha Tamiym Ad Daariyy (Radhwiya Allaah ‘anhu) alichokihadithia kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:  “Dajjaal alisema:  Hakika mimi ni Al-Masiyh Ad-Dajjaal, na muda umekaribia niruhusiwe kutoka.  Nikitoka nitatembea dunia yote, siachi mji wowote isipokuwa nitatuwa hapo katika muda wa siku 40, ila Makkah na Madiynah.  Miji yote hiyo miwili ni marufuku kabisa kwangu.  Kila nitakavyojaribu kuingia kwenye mji mmoja kati ya hiyo miwili, atanikabili Malaika mwenye upanga uliochomolewa anizuie kuingia, na katika kila kona na njia ya miji hiyo kutakuwa na Malaika wanalinda.  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akagonga mimbari kwa fimbo yake na kusema:  Huu ni Twaybah, huu ni Twaybah, huu ni Twaybah”.  [Swahiyh Muslim: 2942]

Twaybah ni Madiynah.

 

 

Share