04-Tukumbushane: Mtoto Ni Neema

 

Tukumbushane

 

Alhidaaya.com

 

 

04:  Mtoto Ni Neema:

 

 

Ni neema pale utakapomlea vyema.  Kila jema atakalolifanya, basi pia linawekwa kwenye mizani za wazazi wake wawili waliomlea na kumfundisha au yeyote aliyesimamia ulezi wake.  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatuambia:

 

"إنَّ الرَّجلَ لتُرفَعُ درجتُه في الجنةِ فيقولُ : أنَّى هذا ؟ فيقالُ : باستغفارِ ولدِك لكَ"

 

“Hakika mtu atakuta daraja zake zimenyanyuliwa Peponi aseme:  Zimekujaje hizi? Ataambiwa:  Ni kutokana na duaa za wanao za kukuombea maghfirah”. [Hadiyth Hasan.  Swahiyh Ibn Maajah]

 

Mtoto ni rasilimali nzuri.  Iwekeze vyema ikufae duniani na aakhirah.  Usijali gharama unazotoa kwa ajili ya hilo.  Zote zitarudi na ziada teletele.

                             

 

Share