06-Tukumbushane: Ulimi Ni Maafa

 

Tukumbushane

 

Alhidaaya.com

 

 

06:  Ulimi Ni Maafa:

 

 

Ulimi unaweza kuwa ni maafa kwa mwanadamu kama ambavyo unaweza pia kuwa ni sababu ya kuingia Motoni kutokana na neno moja tu au tamshi moja tu.  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"‏إِنَّ الرَّجُلَ لَيَتَكَلَّمُ بِالْكَلِمَةِ لاَ يَرَى بِهَا بَأْسًا يَهْوِي بِهَا سَبْعِينَ خَرِيفًا فِي النَّارِ ‏"‏ 

 

“Kwa hakika mtu anaweza kutamka neno ambalo haoni madhara yoyote kwalo akaja kuporomoka nalo motoni majira 70 ya vuli (miaka 70)”.  [Hadiyth Hasan Ghariyb.  Imesimuliwa na Abu Hurayrah]

 

Linaweza kuwa neno litakalochemsha ghadhabu za Allaah na mtu akaliona halina uzito wowote.  Uso wa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ulitaghayuri kwa hasira wakati Bibi ‘Aaishah alipomtia kasoro Bi Swafiyyah kwa neno linalomaanisha kuwa ni mfupi.  Rasuli akamwahi hapo hapo na kumwambia:

 

"لقدْ قلتِ كَلِمَةً لَوْ مُزِجَتْ بماءِ البحْرِ لَمَزَجَتْهُ"

 

 “Hakika umetamka neno ambalo lau lingechanganywa na maji ya bahari basi lingeyachafua yote (kutokana na ubaya wake)”.  [Swahiyh Al-Jaami’u. Imekharijiwa na Abu Daawuwd]

 

Tutahadhari sana na ndimi zetu.  Allaah Atusamehe madhambi yetu ya ulimi na Atujaalie tuyaepuke.

                                                  

 

Share