10-Tukumbushane: Thawabu Kubwa Kwa Huduma Ndogo

 

Tukumbushane

 

Alhidaaya.com

 

10:  Thawabu Kubwa Kwa Huduma Ndogo:

 

Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:

 

"مَن مَنحَ منِيحةَ لبنٍ أو وَرِقٍ أو هَدَى زِقاقًا كانَ له مثلُ عتقِ رقَبَةٍ"

 

“Mwenye kutoa mnyama wa kukamwa maziwa, au mkopo wa fedha, au akamwelekeza mtu njia au sehemu, basi atapata (thawabu za) mfano wa kumwacha huru mtumwa”.  [Imesimuliwa na Ahmad, Al-Bukhaariy na At-Tirmidhiy]

 

Kuwasaidia watu na kuwapa, ni katika sifa njema ambazo Muislamu anatakikana ajipambe nazo na kujipambanua kwazo na wengineo.  Na hii ni kutokana na malipo makubwa yaliyomo ndani yake.

 

Kadhalika, kumwelekeza mtu njia au sehemu anayotaka kwenda, thawabu zake ndio kama hizo.  Jambo hilo tunaliona dogo, lakini mbele ya Allaah ni kubwa.

 

Hivyo, tusidharau jema lolote hata kama kwa akili zetu tutaliona ni dogo vipi.

                                    

 

Share