12-Tukumbushane: Mwanaume Usivae Hariri, Utaikosa Ya Peponi

 

 

Tukumbushane

 

Alhidaaya.com

 

 

12:  Mwanaume Usivae Hariri, Utaikosa Ya Peponi:

 

Kujinyima na kujizuia na makatazo leo hapa duniani, ni jambo jepesi zaidi kuliko kesho Aakhirah.  Nadhani ndugu yangu Muislamu umeisikia Hadiyth ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo:

 

"مَنْ لَبِسَ الْحَرِيرَ فِي الدُّنْيَا لَمْ يَلْبَسْهُ فِي الْآخِرَةِ"

 

“Mwenye kuvaa hariri duniani, hatoivaa akhera”.

 

Na ‘Abdullaah bin Az-Zubayr akaongezea kauli yake:  “Na ambaye hatoivaa Aakhirah, basi ina maana haingii Peponi”.

 

Hivyo basi mwenye kunywa pombe ya dunia, hatokunywa ya Peponi, na mwenye kuwaangalia kwa matamanio wanawake basi kesho atanyimwa kuwaangalia wanawake wazuri wa Peponi wenye macho makubwa Mahuwr Al Ayn, na mwenye kusikiliza miziki, hatosikiliza ya huko.

 

Zuio hili kwa mujibu wa maneno ya ‘Abdullah bin Az-Zubayr, linamaanisha kuwa mtu haingii Peponi akayapata hayo kutokana na kujiachilia nayo hapa duniani.  Na huu ni msiba mkubwa.  Na hii pia inaingia ndani ya wigo wa kudharau madhambi na matokeo yake.

 

Lakini ‘Ulamaa wanasema kuwa ataingia Peponi kwa mujibu wa mizani yake ya matendo, lakini humo hatopata tembo la huko au kuvaa Hariri.  La muhimu mtu ajiepushe na maharamisho yote kiasi awezavyo.

                    

 

Share