13-Tukumbushane: Allaah Hufurahika Kwa Toba Yako Lakini Shetani Hununa

 

Tukumbushane

 

Alhidaaya.com

 

 

13:  Allaah Hufurahika Kwa Toba Yako Lakini Shetani Hununa:

 

Ndugu Muislamu!  Jua kwamba unapotubia kikweli, basi Allaah Anafurahi, Malaika hukufurahikia na shaytwani hughadhibika mno.  Isitoshe, daftari lako huwa safi bila tone ya dhambi, daraja yako hupandishwa na hadhi yako huwekwa juu.  Lakini pia baraka hukuteremkia, matatizo uliyonayo huondoka, na moyo wako hupata utulivu.  Hayo yote ni kwa ajili tu ya toba yako nailhali wewe ulikuwa mkosa.  Na wewe ni nani hata Allaah Afurahi kwa toba yako!  Ni neema iliyoje hiyo!  Na kwa ajili hiyo, asiyetubu kwa Allaah, basi huyo ni katika madhalimu.  Allaah Anasema:

 

"وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ"

 

“Na yeyote asiyetubu, basi hao ndio madhalimu”.  [Al-Hujuraat: 11]

 

Mizani yako itawekwa mbele ya macho yako Siku ya Qiyaamah.  Mema yako yatawekwa kwenye mkono mmoja wa mizani na mabaya kwenye mkono mwingine.  Hakuna njia ya kuufanya mkono wa mema kuwa mzito isipokuwa kwa toba njema ya kufuta mabaya hayo.  Usikawie hata kidogo kuacha mabaya hayo kubaki kwenye daftari lako.

                                                             

Share