15-Tukumbushane: Je, Haujafika Tu Muda Wa Wewe Kujionea Haya Na Nafsi Yako?

 

Tukumbushane

 

Alhidaaya.com

 

 

15:  Je, Haujafika Tu Muda Wa Wewe Kujionea Haya Na Nafsi Yako?

 

Yaonee haya masikio yako, macho yako na ngozi yako.  Viungo hivi Allaah Amevifanya kuwa kama ni majasusi wanaokuona popote unapokwenda, na ndivyo vitakavyotoa ushahidi dhidi yako mbele ya Allaah na mbele ya kizingiti cha Jahannam.

 

Allaah Anasema:

 

"حَتَّىٰ إِذَا مَا جَاءُوهَا شَهِدَ عَلَيْهِمْ سَمْعُهُمْ وَأَبْصَارُهُمْ وَجُلُودُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ"

 

“Mpaka watakapoufikia, yatashuhudia dhidi yao masikio yao, na macho yao, na ngozi zao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda”.  [Fusswilat: 20]

 

Viungo vyako vinaona na kusajili kila tendo lako, na Siku hiyo vitatoa ushahidi dhidi yako kwa kila dogo na kubwa unalolifanya sasa.  Kujua hili ni chachu ya kukufanya ujiepushe na makatazo.  Hivyo basi, jionee haya mwenyewe kwa nafsi yako kumwasi Allaah, kwani viungo vyako mwenyewe vinakuona, Allaah Anakuona, na Malaika Wake wanasajili kila kitu.

 

 

 

Share