23-Tukumbushane: Kuamsha Watoto Kuswali

 

Tukumbushane

 

Alhidaaya.com

 

 

 

23:  Kuamsha Watoto Kuswali:

 

Swalaah ni ‘ibaadah kati ya ‘ibaadah bora kabisa ambayo wengi wetu wanaifanya lakini pengine hawajui ubora wake.  Kuwaamsha watoto na hususan kwa ajili ya Swalaatul Fajr na kuwazoesha Swalaah kiujumla tokea udogoni, ni moja ya ‘ibaadah bora kabisa.  Kwa ‘ibaadah hii, Allaah Amemwamuru Nabiy Wake Muhammad (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Akimwambia:

 

"وَأْمُرْ أَهْلَكَ بِالصَّلَاةِ وَاصْطَبِرْ عَلَيْهَا ۖ لَا نَسْأَلُكَ رِزْقًا ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكَ ۗ وَالْعَاقِبَةُ لِلتَّقْوَىٰ"

 

Na amrisha ahli zako Swalaah, na dumisha uvumilivu juu ya mazito yake. Hatukukalifishi riziki, bali Sisi Ndio Tunaokuruzuku.  Na khatima njema ni kwa wenye taqwa”.  [Twaahaa: 132]

 

Na kuhusu Nabiy ‘Ismaa’iyl Amesema:

 

"وَكَانَ يَأْمُرُ أَهْلَهُ بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ وَكَانَ عِندَ رَبِّهِ مَرْضِيًّا"

 

Na alikuwa akiwaamrisha ahli zake Swalaah na Zakaah, na alikuwa mridhiwa mbele ya Rabb wake”.  [Maryam: 55]

 

Na wasiya wa Luqmaan kwa mwanaye:

 

"يَا بُنَيَّ أَقِمِ الصَّلَاةَ"

 

“Ee mwanangu! Simamisha Swalaah”.  [Luqmaan: 17]

                    

                                                             

Share