41-Tukumbushane: Na Fisi Je?

 

Tukumbushane

 

Alhidaaya.com

 

 

 

41:  Na Fisi Je?

 

Naam, fisi naye anafaa kwa kitoweo.  Pengine wengi watashangaa, lakini huu ndio ukweli kwamba nyama yake ni halali kuliwa.  Na hii ni kwa  Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdullaah ambaye amesema:   Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu fisi.  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:

 

"هُوَ صَيْدٌ وَيُجْعَلُ فِيهِ كَبْشٌ إِذَا صَادَهُ الْمُحْرِمُ"

 

“Ni mnyama wa kuwindwa, na hufidiwa mahala pake beberu la kondoo kama aliyevaa ihramu atamwinda”. [Hadiyth Swahiyh.  Sunan Abiy Daawuwd].

Kama asingelikuwa halali, basi Rasuli asingelimfanya kondoo kuwa  fidia kwa muhrim aliyemwinda  fisi, na asingeliruhusu kumwinda kwa mchezo tu kama asingelikuwa halali.  Kadhalika, Hadiyth hii ni mahsusi kwa fisi ikimvua toka kundi la wanyama wenye meno na makucha makali walioharamishwa kuliwa.

 

Ash-Shaafi’iy (Rahimahul Laah) amesema katika “Al-Ummu” (2/273):

 

“Na nyama za fisi zinauzwa kwetu Makkah kati ya Swafaa na Marwa, simjui yeyote katika watu wetu ambaye amepinga uhalali wake”.

 

Hivyo basi, fisi ni halali nyama yake bila makhitilafiano yoyote kati ya ‘Ulamaa.

 

 

 

Share