43-Tukumbushane: Na Nyoka Je?

 

Tukumbushane

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

43:  Na Nyoka Je?

 

Nyoka ni haramu kuliwa.  Na hii ni kwa sababu mbili:

 

Ya kwanza:  Kanuni ya kifiqhi inasema:

 

“Mnyama Ambaye Rasuli Kaamuru Kumuua Si Halali Kuliwa”.

 

Na kwa msingi huu, nyoka ni haramu kuliwa kutokana na Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) ambaye amesema:

 

" كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ فِي غَارٍ وَقَدْ أُنْزِلَتْ عَلَيْهِ :‏ ( وَالْمُرْسَلاَتِ عُرْفًا)‏ ‏.‏ فَنَحْنُ نَأْخُذُهَا مِنْ فِيهِ رَطْبَةً إِذْ خَرَجَتْ عَلَيْنَا حَيَّةٌ فَقَالَ : ‏"‏ اقْتُلُوهَا ‏"‏‏، فَابْتَدَرْنَاهَا لِنَقْتُلَهَا فَسَبَقَتْنَا ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ : ‏"‏وَقَاهَا اللَّهُ شَرَّكُمْ كَمَا وَقَاكُمْ شَرَّهَا‏"‏ ‏.‏

 

“Tulikuwa pamoja na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika pango akiwa ameshateremshiwa (Wal Mursalaat ‘Urfan).   Na wakati tukiwa tunaisikiliza (suwrah) toka mdomoni mwake ikiwa bado mbichi mpya, mara ghafla akatutokezea nyoka mkubwa, na Rasuli hapo hapo akatuambia: “Muueni”.   Tukakimbizana haraka tuwahi kumuua lakini akawahi kutukimbia. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa sallam) akasema:  Allaah Amemlinda na shari yenu kama Alivyowalindeni nyinyi na shari yake”.  [Swahiyh Muslim (2234)]

Ya pili:   Nyoka ana meno anayotumia kuulia kiwindwa chake, ni sawa kwa kumdunga sumu, au kukamatia nayo.  Hivyo anaingia kwenye kundi la wanyama wenye meno kwa mujibu wa Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas:

 

"نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلًى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ عَنْ ُ َكُلِّ ذِيْ نَابٍ مِنَ السِّبَاعِ، وَعَنْ كُلِّ ذِيْ مِخْلَبٍ مِنَ الطَّيْرِ"

 

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kila mwenye meno katika wanyama wakali, na kila mwenye kucha katika ndege”.  [Hadiyth Swahiyh.   Imekharijiwa na Muslim (1934), Abu Daawuwd (3785) na An Nasaaiy (7/206)].

 

Hivyo nyoka si halali kuliwa; si wakubwa wala wadogo.

 

 

 

Share