03-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Posa Na Hukumu Zake:Inajuzu Walii Kumtangazia Bintiye Kwa Watu Anaowaona Kuwa Wana Vigezo Vya Kumwoa

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا

 

Posa Na Hukumu Zake

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

03:  Inajuzu Walii Kumtangazia Bintiye Kwa Watu Anaowaona Kuwa Wana Vigezo Vya Kumwoa:

 

1-  Mzee mwema alimwambia Muwsaa ‘Alayhis salaam:

 

"قَالَ إِنِّي أُرِيدُ أَنْ أُنكِحَكَ إِحْدَى ابْنَتَيَّ هَاتَيْنِ عَلَىٰ أَن تَأْجُرَنِي ثَمَانِيَ حِجَجٍ"

 

“Akasema:  Mimi nataka nikuozeshe mmojawapo wa binti zangu hawa wawili kwa sharti kuwa unitumikie miaka minane”.  [Al-Qaswas: 27]

 

2-  Katika Swahiyh, ni kwamba ‘Umar bin Al-Khattwwaab wakati binti yake Hafswah alipoondokewa na mumewe Khunays bin Hudhaafah As-Sahmiy, alimdokezea kwa ‘Uthmaan, kisha kwa Abu Bakr, na hatimaye Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwoa.  [Imechakatwa na Al-Bukhaariy (5122)]

 

3-  Ummu Habiybah alisema:

 

"يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَنْكِحْ أُخْتِي هَمْنَة بنت أبي سُفْيَان، فَقَالَ: أَوَ تُحِبِّينَ ذَاكَ؟‏ ‏‏قَالَتْ: نَعَمْ، لَسْتُ بِمُخْلِيَةٍ بِكَ، وَأَحَبُّ مَنْ شَارَكَنِي فِي خَيْرٍ أُخْتِي.‏ قَالَ: ‏فَإِنَّهَا لاَ تَحِلُّ لِي"

 

“Ee Rasuli wa Allaah!  Mwoe dada yangu Hamnah bint Abiy Sufyaan.  Rasuli akamuuliza:  Unaridhia hilo?  Akasema:  Na’am, mimi si mke pekee kwako, nina wake wenza wenzangu, na  mtu ambaye ningependa zaidi ashirikiane nami katika kheri hii ni dada yangu.  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:  Huyo kwangu si halali”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imechakatwa na Al-Bukhaariy (5101) na Muslim (1449)]

 

4-  ‘Aliy bin Abu Twaalib amesema:

 

"قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَا لِي أَرَاكَ تَنَوَّقُ فِي قُرَيْشٍ وَتَدَعُنَا؟ قَالَ: عِنْدَكَ شَيْءٌ؟ قُلْتُ: بِنْتُ حَمْزَةَ، قَالَ: هِيَ بِنْتُ أَخِي مِنَ الرَّضَاعَةِ‏"

 

“Nilimwambia (Rasuli wa Allaah):  Ee Rasuli wa Allaah!  Mbona umelalia zaidi upande wa Maquraysh na sisi unatusahau!  Akauliza:  Je, una yeyote? Nikasema:  Na’am, binti wa Hamzah.  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:  Huyo ni binti wa kaka yangu wa kunyonya”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imechakatwa na Muslim (1446) na An-Nasaaiy (6/99)]

 

 

 

Share