04-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Posa Na Hukumu Zake:Mwanamke Anaruhusiwa Kisharia Kujinadia Mwenyewe Kwa Mtu Mwema Ili Amwoe

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا

 

Posa Na Hukumu Zake

 

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

04:  Mwanamke Anaruhusiwa Kisharia Kujinadia Mwenyewe Kwa Mtu Mwema Ili Amwoe:

 

1-  Toka kwa Anas, amesema:

 

"جَاءَتِ امْرَأَةٌ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ تَعْرِضُ عَلَيْهِ نَفْسَهَا، قَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ أَلَكَ بِي حَاجَةٌ؟ فَقَالَتْ بِنْتُ أَنَسٍ: مَا أَقَلَّ حَيَاءَهَا، وَاسَوْأَتَاهْ وَاسَوْأَتَاهْ‏.‏ قَالَ أَنَسٌ: هِيَ خَيْرٌ مِنْكِ، رَغِبَتْ فِي النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَعَرَضَتْ عَلَيْهِ نَفْسَهَا"

 

“Mwanamke mmoja alikuja kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ili kujitambulisha mwenyewe kwake.  Akamwambia:  Ee Rasuli wa Allaah!  Je, unanihitajia (niwe mkeo)?  Binti ya Anas akasema:  Kakosa haya kiasi gani mwanamke huyu!  Aibu! Aibu!  Anas (Radhwiya Allaah ‘anhu) akamwambia:  Yeye ni bora kukushinda wewe.  Amepata utashi kwa Rasuli na akamweleza bayana dhamira yake”.  [Swahiyh.  Al-Bukhaariy (5120), An-Nasaaiy (6/78) na Ibn Maajah (2001)]      

 

2-   Toka kwa Sahl bin Sa’ad, amesema:

 

"أَنَّ امْرَأَةً عَرَضَتْ نَفْسَهَا عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ لَهُ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللَّهِ زَوِّجْنِيهَا‏"

 

“Kwamba mwanamke mmoja alijielezea mwenyewe kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam).  Na hapo mtu mmoja akamwambia:  Ee Rasuli wa Allaah!  Niozeshe mimi (kama humtaki)”.  [Swahiyh.  Al-Bukhaariy (5126) na Muslim (1425)]

 

Hili mwanamke atalifanya kama hakuna fitnah au tatizo lolote.  Na kama itakuwepo kama atamweleza mwanaume utashi wake wa kuolewa naye, basi haitojuzu. 

 

"وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ"

 

“Na Allaah Hapendi ufisadi”.  [Al-Baqarah:  205]

 

 

 

Share